MSAADA: Nasumbuliwa na miguu kuuma, hasa mguu wa kushoto

MSAADA: Nasumbuliwa na miguu kuuma, hasa mguu wa kushoto

Pamoja na kutafuta matibabu, fanya yafuatayo:
1. Acha kabisa kunywa vinywaji vyenye sukari kama vile juice, soda na bia laini
2. Acha kula wali, ugali, mikate
3. Kula vyakula vya protini kwa wingi, huko huko utapata carbohydrates za kwenye ugali na wali.
4. Kula mboga mboga
Shukrani
 
Hilo ni tatizo la mishipa ya fahamu.
Nenda kwenye hosipitali kubwa zenye wataalam wa fani hiyo utatibiwa na utapona kabisa.

Pole sana!
Leo nilikuwa na mzee mmoja akaniambia miaka kama7 nyuma alisumbuliwa na hili tatizo anasema kipindi yupo arusha alikwenda hospital moja anakwambia tena ndogo tu,wakamfanyia vipimo vya Culture blood sijui alitamka sawa akiwa anamaanisha kwamba walipandikiza damu baada ya siku tatu wakampa majibu ya .......!!!

Kwamba tatizo lake lilitokana na kula siagi,maziwa na nguruwe sasa baada ya kumpa dawa amepona mpaka leo,ila alochoaema ni miaka mingi huko Arusha.

Ndio nataka kujua hospital gan wanaweza toa hiyo huduma ya blood Culture sijui aliamka sahihi
 
UPDATE---
Nimekwenda mwananyamala nimefanya kila aina baadhi ya vipimo na kusema kwamba MISULI IMEKAZA.

Hivyo nimepata dawa,naingia wiki la pili sasa lakin naona nafuu hamna au ngoja tuendelee kufuta subra
 
Nasumbuliwa na miguu kuuma hasa wa kushoto, hivi karibuni nikasogea kwenye zahanati wakaniambia kwamba huo mguu hauumi isipokuwa una ganzi.

Basi wakanifungashia dawa fulani hivi za NATB, ila mguu unauma sana kwenye vidole pindi unapotembea.

Yaani kuanzia kwenye vidole hadi kwenye vigimbi wakati wa kutembea napata shida haswa.

Hivyo basi mwenye kujua, kufahamu wapi naweza pata tiba au nini cha kufanya waweza share nami.

Asanteni.
Habari!
Unaweza kueleza:
1: Uzito wako?

2: Kazi yako kama ni ya kusimama mrefu?

3: Umbali unaitembea kama ni mrefu sana kwa siku?

4: Aina ya vuatu unavyovaa kama vinabontea unapokanyagia/soli au vigumu?

5: Maumivu yako yaliazia wapi? Kwenye kiaigino au katikati ya unyayo?
 
Back
Top Bottom