Msaada: Nasumbuliwa na tatizo la Asidi Tumboni

Msaada: Nasumbuliwa na tatizo la Asidi Tumboni

Jamani naumwa asidi tumboni nimebadilisha mfumo mzima wa maisha dawa nimetumia lakini wapi
Naumwa kifua, mabega maumivu yanasambaa mpaka kwenye maziwa yaani sina raha, ninapata stress hamu ya tendo imepungua anayejua dawa ya kienyeji msaada
Nashauri utumie kwa wingi sana vyakula vyenye asili ya ALKALI kama vile mboga za majani (mchicha, spinach na nyinginezo ila isiwe kisamvu), matunda kama parachichi, pera na mapapai)
Tumia juice ya tango na bamia.
Tumia mwani (sea moss).
Ukifanya hivi utakuja kunishukuru.
Kwa kipindi hiki epuka kabisa vyakula vyote vyenye asili ya asidi.
USHAURI:
Kwa wengine ambao hatuna tatizo hili nashauri tutumie vyakula hivi kwa sehemu kubwa ya milo yetu.
 
Tatizo lako ni indigestion!!!

Vidonge havitkusaidia!!

Chai au kahawa isiyo na sukari has kahawa chungu itakusaidia yaani deep roasted coffee with too much caffeine!

Tafuta hiyo chemsha na uwe unakunywa walau vikombe viwili asubuhi kabla hujala chochote na usiku baada ya kula!!

Achana na soda kabisa!!
 
Anza na kutengeza juice ya cabbage ๐Ÿฅฌ,kunywa glasi moja asubuhi kabla hujaja kitu na jioni unapoenda kulala. Kata cabbage,weka kwenye blender na maji kidogo na usiichuje,kunywa hivyo hivyo. Pia hakikisha unakunywa juice ambayo haijakaa zaidi ya masaa 48 kwenye friji.

Hii juice kunywa mwezi mzima kisha leta mrejesho hapa. Baada ya hapo unaweza kuhamia kwenye bidhaa nyingine za kukusaidia kuendelea kupata unafuu mpaka uone
 
Back
Top Bottom