Msaada: Natafuta shule nzuri za Sekondari

Msaada: Natafuta shule nzuri za Sekondari

Rene Jr.

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2014
Posts
3,714
Reaction score
2,376
Habari wakuu. Kijana wangu anaandika mtihani wa darasa la saba wiki ijayo.

Najaribu kutafuta na kulinganisha shule za sekondari kwa ajili yake. Anapenda sana masomo ya sayansi, hasa kwa vitendo, hivo ningependa shule ambayo wana ubunifu wa sayansi, hasa clubs hai za ushindani na walimu wenye uwezo bila kusahau maabara zenye vifaa.

Ada isizidi milioni 4 kwa mwaka. Natumaini jukwaa hili lina watu wengi wenye uelewa huo naweza kusaidika.

Natanguliza shukrani.
NB: Shule iwe ya bweni, ni mvulana
 
Uwezo anao?

Maana private za maana hawabebi mizigo, usipopita interview hawana muda na ww hata uwe na pesa vipi.... mkianza kusoma ukiwa una underperform pia wanakuchomoa...
 
Back
Top Bottom