Magazine ni jarida, gazeti ni newspaper. Kuna tofauti kati ya magazine na gazeti, but anyway nenda ofisi za IDARA YA HABARI MAELEZO utapewa utaratibu kamili. Gharama ya kusajili gazeti au magazine ni shilingi LAKI TANO.
UTARATIBU KAMILI UPO HIVI :
1. Unaandika barua ya maombi ya usajili wa gazeti/jarida kwa MSAJILI, IDARA YA HABARI MAELEZO.
2. Viambatanisho ;
i. Jina la biashara ( Sole Proprietorship ) au jina la kampuni kama una miliki kampunu, pamoja na certificate ya usajili wa jina la biashara au kampuni kutoka BRELA.
iii. Utapendekeza majina kuanzia matatu ambayo utapenda gazeti/jarida lako liitwe
iv. Taarifa za akaunti yako ya benki zinazo onyesha kuwa una uwezo wa kutoa mfululizo wa matoleo kumi ya gazeti lako bila kutegemea chanzo kingine cha mapato .
N.B: Kuhusu taarifa za akaunti usiogope sana, unaweza kueleza kuwa utakuwa unatoa labda nakala mia kwa wiki some thing which means that akaunti yako inaweza ikawa hata na sh laki mbili na bado ukawa na uwezo wa kusajili gazeti lako.. Hope maelezo yangu yatakuwa na msaada kwako. God Bless U