Msaada: Nataka kumpeleka mgonjwa wangu India

Suki

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Posts
373
Reaction score
16
Background: Nina mgonjwa ambaye amekuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu. Katika kipindi chote hicho, aliweza kumanage vidonda hivyo kwa lishe bora na mazoezi ya kujenga mwili. Recently, vidonda vimeibuka na vinamsumbua sana. Alifanyiwa barium x-rays na baada ya kulocate problem area walimpa dawa ya kusaidia kupunguza internal bleeding kutoka kwenye vidonda. Hali ikaimarika kidogo ila vidonda bado vikaendelea kumsumbua na hata kusababisha kupungukiwa damu mwilini. Next step ikawa ni kufanya upper endoscopy kufahamu kama tatizo lilikuwa associated na cancer. Majibu yalionyesha kuwa hana cancer and we were back to square one, vidonda vya tumbo.

Kutokana na tatizo hili kumsababishia kupungukiwa damu mara kwa mara, nimeona ni bora aende kupatiwa matibabu India ili niweze kuwa na amani--na itasaidia pia kuepukana na hofu ya kupungukiwa damu wakati akiwa bila uangalizi.

Swali langu: Nimepewa initial suggestions lakini sio Kwa kina. Nimeambiwa matibabu India ni $10,000 zinazojumuisha usafiri, matibabu yenyewe na therapy. Pia anatakiwa kusindikizwa na daktari wake na msaidizi wa kumwangalia mgonjwa 24/7. Kwa kweli sina ujuzi wowote wa hospitali nzuri India zinazoweza kutibu tatizo hili na ningeomba ushauri wenu kwa hili. Pili, kuna yeyote ambaye ana experience na tatizo kama la mgonjwa wangu anifahamishe ni nini alifanya?

Natanguliza shukrani.
 
pole mkuu ngoja wajuzi waje,
ila hosptal zingine india ni bussiness tu ,ila as long hana cancer atatibika,pigana tu
 
Nimegundua wana matawi mbalimbali ya Apollo na so far ni hili la Indraprastha ndio linaspecialize kwenye gastroenterology (there could be others, not sure yet). Nashukuru sana kwa suggestion, kidogo nimepata mahali pa kuanzia.
Naendelea kuomba suggestions zenu.
 
Appollp kuna ile ya Delhi na AndraPradesh-Hyderabad....so inategemea ticket yako inakwenda wapi...bt hiyo hospital ya AP na huo mji life lake ni kawaida sana kuliko huko delhi. Usiende hospital za Bombay nyingi ni business...bt hizo gharama ulizoambiwa is bit high, labda zikave everything, matibabu, airtickets, maradhi, misosi, shopping nk
 

Kwenye website yao inaonyesha kuwa hii iko New Delhi.
This is what comes up http://www.apollohospdelhi.com/web/
 
Jaribu zilizo south na ni rahisi zaidi....
 
Pale Hyderabad pia kuna hospitali inaitwa MEDWIN. Inao wataalamu wazuri wa Gastroentrology. Nilikuwa pale 1990s
 
Pale Hyderabad pia kuna hospitali inaitwa MEDWIN. Inao wataalamu wazuri wa Gastroentrology. Nilikuwa pale 1990s

Nitaiangalia na hii pia, kwa kupitia tu tovuti yao nimeona kuwa wanaspecialize kwenye gastroenterology which is in itself encouraging. Asante sana.
 
Pale Hyderabad pia kuna hospitali inaitwa MEDWIN. Inao wataalamu wazuri wa Gastroentrology. Nilikuwa pale 1990s

Napata tatizo kidogo kutokana na tovuti yao kutotoa maelezo zaidi kuhusu in patient facilities zao. Nadhani kwa mgonjwa ambaye kuna uwezekano mkubwa akafanyiwa operation, information kuhusu facilities ni muhimu sana. Ninaendelea kuperuzi lakini, I figured you would appreciate some feedback.
 
Mkuu usihangaike sana kwenda india wala hospital za kisasa kwani wengi wataishia kukata utumbo au kukupa dawa za muda mfupi.Mimi mwenyewe nilisumbuliwa sana na vidonda,baada ya kuhangaika sana nilimpata mzee mmoja anatibu kwa kutumia dawa za asili anachanganya na asali mbichi.Alinitibu mwaka 2008 na nilipona kabisa.Pia watu wengi niliyowarefer kwake wamepona.Yupo Mtoni Madafu,Dar,mtafute namba yake ni 0774553650
 
Pole sana mkuu, nimehangaika sana india na mama yangu miaka miwili iliyopita..

india kuna hospitali nyingi kwa watu wengi wanaisifia sana apollo main hospital ambayo ipo hyderabad city huko andhra pradesh state south india.. Jamaa ni wazuri sema wameweka pesa mbele sana...

Ukifika appollo first utaambiwa udeposit usd 5000 kwa ugonjwa wa design hiyo ambayo itaanza kuwa deducted wakati mgonjwa anaendelea kutibiwa ikipungua tu as bills unaziona kwenye management system unadeposit tena hadi mgonjwa wako atakapomaliza matibabu..

Ni vizuri ukifanya research ya gharama za huo ugonjwa matibabu yake kabla hujasafiri ujiandae kwa mawasiliano kwa international division wa appollo health city anaitwa Rokesh ndo atakushauri vizuri uende appollo ya wapi na uwe na kiasi gani..

Na pia gest house in jubilee hills, hyderabad ilipo appollo sio expensive kivile kwa usd 20 unapata place nzuri kibao sema chakula ndo hakipandi. Ila kuna migahawa mikubwa duniani as mac donald na KFC restaurant zipo jirani na jubilee hills na bei ni affordable hawa wanapika international foods,, na vile vile appollo health city ina restaurant ndani ya hospital inapika vyakula vyote kwa bei nzuri.. Ila mgonjwa anapikiwa anachotaka kula kwa bei ile ile ya matibabu,, msos wake unakuwa included na anakula msos mzuri wa kitanzania..

Pia mgonjwa akilazwa apollo hospital rum ya bei rahisi ni almost usd 160 per day international pavillion sema ina world class facilities kuanzia vifaa, flat screens, phones, internet access, washrooms with heater etc, na manesi wapo wengi sana wa kumshughulikia mgonjwa kwa apollo hata ukienda na nurse hata kuwa na kazi wana nurse wengi na wanajua kazi yao sana..

Pia kuna options nyingine called narayana health city in bangalore napo ni among best hospital in south asia yaani bonge la hospital sema tatizo la hawa wapo busy sana wagonjwa mnakuwa treated as outpatient tulifika huko na b mkubwa kwa ajili ya radiotherapy na tulikuwa refered na aghakhan headquarter in Mumbai,, hawa Narayana bei zao atleast ni nzuri na wana specialist wa kumwaga..


Kuna nyingine ipo Mumbai,, indias biggest city.. Inaitwa agakhan prince alikhan ambapo ndo worldwide aghakhan head quarter nao wazuri..

Njia nzuri ya kujua gharama ni kuwasiliana na international division za hospital kubwa huko watakuunganisha na consultant wao through e mails na watam review mgonjwa online kwa kuchek progress yake, matibabu aliyofanyiwa bongo, vipimo vyake watavicheki then watakushauri cha kufanya...

All in all wahindi wapo serious na wana World class facilities kwenye hospital zao na hizo ndo zinawabeba,, nina imani hata Tanzania hospitali zikipata facilities hizo na ma Dr na manesi wa tz wafanyishwe kazi kwa KPI lazima tungewafikia... Maana kule hadi nurse anajaza KPI kwenye nurse station kwa kila anachofanya na kuna appraisal na wakati mgonjwa unakuwa discharged mnajaza fomu za maoni na mkiamua kuponda huduma zao waliowahudumia wataipata


Angalizo wahindi wajanda na wanapenda sana hela hizi hospitali ndogo ndogo hata kama ugonjwa hawauwezi au umefika pabaya wao watakupokea wale hela yako tu na kumfanyia mgonjwa surgery ya kiushahid mradi wapate hela... So kuwa mwangalifu kaka
 
Pole sana:

Huyo mgonjwa wako kama kweli ana ulcers zinazobleed ni hali ya hatari. Normally bleeding ulcers may lead into something serious. Pia kuambiwa kuna hana dalili za kansa kwa hapa kwetu inaweza kuwa misleading . Hivyo nakushauri ufanye njia madhubuti aende kutibiwa mapema.

Mimi nilikuwa nasumbuliwa na vidonda vya tumbo for the past 15 years (Duodenal Ulcers), na vilikuwa vikianza hata kitandani silali-ni maumivu, moto, kutapika , mgongo unauma (pain radiates to other parts ) and so forth. Hata wali ,pilau, viungo vyote nilikuwa situmii. Nilifanyiwa barium meal test Hindu Mandal na Muhumbili na kupewa treatment (Heligo Kit+ omeprazole tabs) na kweli nikapoa for 4 years.

Baadae vikazuka na nilipoenda Regency wakasema nifanye endoscopy. Bahati kuna nesi alishauri nisifanye hicho kipimo (so painfull I guess+expensive). So i resorted to go to India kwa normal checkup na haikuwa official maana nilienda kama holiday then nikasearch from wenjeji where I can get treated. To cut the story short- Nilipofika hosp Delhi (Br Kapur Speciality hosp) nilipata reception nzuri ajabu, na iligundulika kuwa my cancer was almost going to need surgery (kukata the most infected part of the duodenum. Kwa hospitali Nilitumia dola 1700 hii ikijumuisha consultation, full body checkup, medicine, vipimo vyote (scan, ECO, etc). Gharama za kuishi India ni ndogo sana na pia hosp wanatake care kila kitu na nilijiweka sawa kuwa kama watanilaza basi nitahudumiwa na manesi wa hapo hapo maana wako extra serious. Namshukuru Mungu niliwekwa mapuziko siku mbili tu na kuendelea na dawa kama kawaida for 14 days na nyingine nikabeba kurudi nazo.

Tangu 2011 sijapata tatizo lolote na unlike huko nyuma nakula kila kitu.

Ninachojaribu ku-drive at here ni kwamba kama ulcers zimefika into bleeding stage please, please don't waste any further minute.

Fana internet search ya kutosha , pia tumia wadau hapa ambao wako experienced na hosp na miji tofauti. Na kama unahisi mgonjwa anaweza kuwa operated tafuta miji yenye unafuu (sio Delhi).
 

Asante mkuu ila kuna kipindi alishauriwa amwone daktari mmoja (I'm spacing out on her name) ambaye aliambiwa anatibu kwa dawa za kienyeji na kwa kweli sikufurahishwa na outcome. Mgonjwa alitakiwa anywe gallons za hiyo dawa na badala ya kupata nafuu, kila anapomaliza vikombe viwili vitatu, anakuwa nyang'anyang'a na kukosa nguvu kabisa. Tangu kipindi hicho nimekuwa mwoga sana na hizi alternative medicines hapa nyumbani.
 

Nashukuru sana kwa maelezo yako ya kina. Katika moja ya tovuti za Apollo, wameonyesha kuwa pia wanatoa e-consultations kwa wagonjwa walioko mbali, nadhani hii itakuwa mwanzo mzuri katika maandalizi ya awali kabla ya safari ili mgonjwa atakapofika, hatasumbuliwa tena on background info.

Unakumbuka position ya Rokesh iliitwaje? Najaribu kutafuta kwenye tovuti ya Apollo Health City mtu anayehusika na international patients na ninampata senior general manager tu. Hii ya Hyderabad wana helpline kwa ajili ya international patients so nitawapigia niwaulize kuhusu gharama zao, average duration ya matibabu na post treatment therapy.

Again, asante sana kwa ushauri.
 

Kwa kweli hata mgonjwa wangu, spicy foods have always been a big no no.
Kidonda kinachomsumbua zaidi kiko right below the cardiac sphincter muscle na hiki ndio kinachobleed from time to time. Hii pia inamsababishia acid reflux na kumpa shida kila anapokula.

Kati ya vipimo vyote, kwa kweli endoscopy is my patient's worst nightmare. Ingawa wanasema ni mildly intrusive the level of discomfort could not get any worse.
Ila kama ulivyosema hali ilipofikia sio wakati tena wa kutegemea updates from regular check ups. Ngoja niongee na hawa watu wa Apollo nisikie wanasemaje.

Asante sana kwa msaada wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…