Msaada: Nataka kupika mlenda, nitafute vitu gani?

Msaada: Nataka kupika mlenda, nitafute vitu gani?

Wasalaam ndugu zangu,
Kuna mboga fulani inaitwa mlenda niliwahi kula zamani kidogo,
inakuwa imelojeka sana. Sasa kutokana na kuisoma namba nataka nijifunze kupika hii kitu ili kubana matumizi. Naomba msaada wa viungo vyake.
Natanguliza Shukrani.
Chukua majani ya mlenda,bamia na karanga zilizopondwapondwa (laini/groundnut paste). Pika kwa pamoja huo mchanganyiko,tonge likikwama njoo univunje shigo.
 
Chukua majani ya mlenda,bamia na karanga zilizopondwapondwa (laini/groundnut paste). Pika kwa pamoja huo mchanganyiko,tonge likikwama njoo univunje shigo.

Mkuu shukrani,
Lakini ni majani ya Maboga au Mlenda?
 
Kuna mlenda wa aina nyingi! Kuna mlenda wa unga ambao waweza weka kwenye maharagwe, kunde, mbaazi, ngogwe na nyanya au mlenda wa majani unaweza changanya Na ngogwe Na nyanya unakuwa Na uchachu kidogo utakula ugali Na kufurahi uwe Na Samaki wa kulumangia hapo
 
.....hahahahaha...unaniangusha mkuda
...opoa goma la kigogo litakufundisha praktikale;
..mi ntakuja na dagaa mchele tutoe kitu cha nguna!
 
Hahahaha wewe mimi Magoma sitaki naogopa sana ngwengwe!
Halafu wewe tangu lini unakula nguna???
Wewe zako si Burger na Pizza???
.....hahahahaha..,mi toka mwanzo,na sasa na siku zote milele mi mtu wa nguna,tena la mtama;we mboga 9 najua unatusorora tu!
....mlenda umekula zamaaaaaaaniiiii,wakati sie tunaula deile neva miss!!
..dagaa mchele unawajua????
 
Back
Top Bottom