Msaada: Nataka kupima/kujua uzito wa nguruwe bila kutumia mizani

emmarki

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,001
Reaction score
1,430
nguruwe akiwa bandani kutambua uzito wake ni shughuli kwa sababu hakuna mizani za kuweza kumpima akiwa hai kwa sababu ni msumbufu.

Naomba kufahamu ni mbinu zipi za kutumia kujua au kupima uzito wa mnyama huyu nguruwe, ili nikimnunua nijue baada ya kutoa utumbo na kichwa angalau nitabaki na kilo kadhaa za nyama. kuangalia kwa macho na kukadiria siwezi.

Watalaamu mje.
 
Mkuu ipo iv nivigumu kujua uzito wa Nguruwe kwa namna unavyo taka wewe lkn ipo ivi asilimia 75 ya uzito wa Nguruwe ni Nyama na 23 ni vitu vya ndani kama vile utumbo, maini , moyo na vinginevyo lkn kwenye upande wa kichwa na kongoro inategemeana na ukubwa pia na aina ya Nguruwe kama ni Large white inaweza kuwa asilimia 3-5 lkn kama ni landrace inakuwa 1-2 lkn Mkuu vitu vyote vya ndani huwa vina tumika kama chakula kwa mwanadamu kwaiyo akuna kinacho tupwa Zaid ya manyoya na kwato [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
angalau hata formula ya kujua uzito wake kwa ujumla
 
Ebu mpige picha alafu tuma maana akuna formula ya icho kitu kwasabubu inategemeana na aina ya Nguruwe, malisho, umli na jinsia
 
1625040543466.png

Uzito = Girth(M)*Girth(M)*Length(M)*69.3 inakuwa na uhakika kwa asilimia 95
 
Kanunue animal weight tape measure inauzwa kwenye maduka ya agrovet.
Hutumika kupima uzito wa ng'ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe kwa kuizungusha kwenye girth ya mnyama.
 
Mdumbukize nguruwe kwenye beseni lililo jaa maji. Kusanya yale maji yatakayo mwagika then uyapime kwa lita. Kila lita ni sawa 0.001m3 . Then zidisha lita za maji yaliyomwagika X 0.001. Then zidisha tena kwa 1000. Hapo utakuwa umepata uzito wa nguruwe
 
mengine yana urefu mita 2 hilo beseni utapata wapi
 
nguruwe akiwa bandani kutambua uzito wake ni shughuli kwa sababu hakuna mizani za kuweza kumpima akiwa hai kwa sababu ni msumbufu.

Naomba kufahamu ni mbinu zipi za kutumia kujua au kupima uzito wa mnyama huyu nguruwe, ili nikimnunua nijue baada ya kutoa utumbo na kichwa angalau nitabaki na kilo kadhaa za nyama. kuangalia kwa macho na kukadiria siwezi.

Watalaamu mje.
Nunua tape measure ya kupima uzito wa nguruwe. Kuna member la advice hapo juu. Ni rahisi Sana kumpima
 
shukarani, naanza kununua na kuchinja hii itanisaidia kukadiria liveweight na nijue jinsi ya kumpasua mfugaji
 
nguruwe akiwa bandani kutambua uzito wake ni shughuli kwa sababu hakuna mizani za kuweza kumpima akiwa hai kwa sababu ni msumbufu.

Naomba kufahamu ni mbinu zipi za kutumia kujua au kupima uzito wa mnyama huyu nguruwe, ili nikimnunua nijue baada ya kutoa utumbo na kichwa angalau nitabaki na kilo kadhaa za nyama. kuangalia kwa macho na kukadiria siwezi.

Watalaamu mje.
Mkuu nguruwe anaangaliwa asubuhi kabla hajalishwa Mimi Nina uwezo wakuangalia tuu na nkakuambia kg zake
 
Back
Top Bottom