Msaada: Nataka kuweka meno ya bandia ya kudumu, inawezekana?

Msaada: Nataka kuweka meno ya bandia ya kudumu, inawezekana?

iron woman

Senior Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
147
Reaction score
19
Habari zenu wadau,

Naomba mnisaidie. Nimewahi kusikia kuwa kuna uwezekano wa kuweka meno ya bandia yakawekewa vyuma yanakuwa siyo ya kutoka tena na ni imara. Naombeni mnijuze, Je hicho kitu ni kweli na kama ndiyo, hiyo huduma inapatikana vizuri hospital gani? Pia mkinisaidia na bei itakuwa vizuri.

Natanguliza shukrani zangu.

Asanteni.
 
Pale mtaa wa msimbaz station ya daladala za kigogona temeke kuna dk wa meno anaitwa akim. Huyu atakusaidia sana anatoa huduma zote hizo
 
Kuna meno bandia aina 2
1.Kuweka na kutoa(removable partial denture )
2.ya kugandishwa na cement maalum. (Fixed partial denture) na kinatokezea kwenye ufizi na kuweza kutengenezewa aina hizo 2 za meno bandia tajwa hapo juu.
Nashawishika unaulizia aina hii ya pili ya meno bandia (fixed denture)ambayo hujulikana zaid kama crown & bridge dental prosthetics

Kuhusu bei
Ina tegemeana na idadi na aina ya material utakayo chagua/tumia.
Angalizo
Implant,kuweka na kutoa na fixed yote yana weza kuwa na chuma.


Hapo kwenye fix ndo kuna chuma mara nyingi panapo tajwa kama meno ya moja kwa moja.
Kuna kitu kina itwa 'implant denture' hapa chuma kina fungwa kwenye mfupa wa mdomo (alveolar bone )
 
Mkuu hata mie nina shida hyo nataka kupandikiza moja la chini mwanzoni niliwekewa ila ni la kuweka na kutoa bahati mbaya fizi yake ilikua kubwa kiac nikawa nashindwa hata kuongea nikalazimika kulitoa
 
Kwa hilo hakuna shida mkuu,fika Muyas dental services ipo pemben na airtel,Morroco. Kuna wataalam wanaingiaga sa 10 jion had sa 1.watakusaidia mkuu
 
Samahan wakuu hatakama nina mwanya naweza Pata jino la bandia la abalone litakuwa permanent kabisaaaa???
 
Asanteni wadau asane MENO Kwa ushauri mzuri mimi nahitaji fixed meno.

Hapa nikihesabu meno mazima kabisa ni 14 na kati ya hayo 18 mengine yashatolewa ni mapengo na mengine ndo yameoza hayafai.
 
Naomba kuuliza, kama mtu hana jino hata moja anaweza kuweka hayo ya kudumu "fixed" kwa wakati mmoja?
Je aina hii ya meno ni imara kiasi kwamba mtu anaweza kutafuna eg nyama ngumu?
 
Asante kwa taarifa ni muda sijaenda Pale wala sijajua kama kahama

Amehama muda nadhani huu utakuwa unaenda mwaka wa pili, alijaribu kuwataarifu baadhi ya wateja naona alokuwa na namba zao
 
Ikishakuwa bandia maana yake ina tegemea na
1.ustadi wa mtengenezaji na 2.utumiaji wa mvaaji.
Kudumu pia inategemeana na mambo hayo 2 hapo juu.
Hata kwa yale orijino kuwa makin pia
 
asanteni wadau asane MENO Kwa ushauri mzuri mimi nahitaji fixed meno.
hapa nikihesabu meno mazima kabisa ni 14 na kati ya hayo 18 mengine yashatolewa ni mapengo na mengine ndo yameoza hayafai

Pole iron woman
Kupata meno fixed ina hitaji meno orijino yalio mazima yachongwe ili kwa kushirikiana na ufizi ya bebe mabovu (ambayo yata fanyiwa tiba ya mzizi)na yale ambayo hayapo.

NB.
Position ya meno mazima ita 'detect' aina ya meno unayo takiwa kuweka.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimeweka jino la permanent pale Agakhan huu ni mwaka wa tano; huwezi kulijua mpaka nikwambie na sijawahi pata tatizo lolote lipo kama meno mengine ila gharama yale ilikua kama milioni mbili mwaka 2011 sasa hivi dola imepanda sina uhakika itakua kiasi gani.
 
Naomba kuuliza, kama mtu hana jino hata moja anaweza kuweka hayo ya kudumu "fixed" kwa wakati mmoja?
Je aina hii ya meno ni imara kiasi kwamba mtu anaweza kutafuna eg nyama ngumu?

Mkuu @ kiranjamkuu
Naomba nikupe taarfa
Kazi kuu ya meno bandia ni
1. Muonekano (aesthetic or appearance)
2. Kufanya Kazi (function)

Mara nyingi meno ya mbele (canine to canine) yana chukua kazi no 1 na yalio baki yanachukua kazi no 2. Ingawa yote yana kazi zote mbili
 
Mkuu @ kiranjamkuu
Naomba nikupe taarfa
Kazi kuu ya meno bandia ni
1. Muonekano (aesthetic or appearance)
2. Kufanya Kazi (function)

Mara nyingi meno ya mbele (canine to canine) yana chukua kazi no 1 na yalio baki yanachukua kazi no 2. Ingawa yote yana kazi zote mbili
mkuu naomba uweke mchanganuo wa hizo bei za meno

mana ninakoenda najiona kibogoyo kabla ya umri
 
Back
Top Bottom