Msaada: Nataka kuzalisha juice (Natural juice), naomba mawazo yenu

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2016
Posts
2,228
Reaction score
2,064
Habari zenu wakuu.

Husika na kichwa tajwa hapo juu, nina Plan za kuanza kuzalisha juice za matunda. Naomba msaada wenu wa mawazo katika nyanja zifuatazo;
  1. Eneo zuri la biashara yaani ofisi itakuwa Dar.
  2. Capital/Mtaji
  3. Mahitaji mengine ya muhimu. Naomba mawazo yenu wadau.
Natanguliza shukrani zangu
 
Mods naomba mu edit hiyo heading badala ya kuzakisha isomeke kuzalisha
 
Kikubwa angalia soko na upatikanaji wa matunda ya kuchuja kiwanda kinatakiwa kuwa kati ya hizo sehemu mbili ila kwa mimi napendelea kiwe sokoni .tafuta
Mashine ya kuoshea
Mashine ya kumenyea
Mashine ya kuchuja/kukamua
Mashine ya kuwekea juice

Ni hayo tuu nazani wengine watachangia vizuri zaidi ya mimi
 
Nashukuru
 
glass(take awaye)- huku mkoani elfu tisa zile zenye mifuniko (zipo sio chini ya sitini)
mirija-huku mkoani elfu sita mia tano ipo sio Chini ya mia mbili
sijajua utauzia kwenye vidumu,mashine,au ndoo
 
glass(take awaye)- huku mkoani elfu tisa(9000/=)zile zenye mifuniko (zipo sio chini ya sitini)
mirija-huku mkoani elfu sita mia tano(6500/=) ipo sio Chini ya mia mbili
sijajua utauzia kwenye vidumu,mashine,au ndoo
 
Juice inalipa Kama ukipata sehem yenye mkusanyiko wa watu Kama kariakoo afu upate pia mtu wa kukutengezea bites Kama sambusa,keki,bagia nk.
 
Ni wazo zuri ..zingatia usafi sehemu yako ya biashara, kingine nionavyo kwa hali ya sasa ukipata frem usitegemee kuuza juice peke yake ,weka chai ya rangi na chai ya maziwa,maziwa fresh na hivyo vitafunio ulivyoshauriwa,kwa maana hiyo unaanza asubuhi mapema wa kubeba take away wanaoenda maofcn,natumai utaweka na viti na meza kwa wateja wako wa hapo hapo,na kwa nje unaweza kuweka kijana wa chips ...inalipa ikiwa utasimama mwenyewe na sio kutegemea wafanyakazi...kila la heri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…