Msaada: Naweza kuua ndege wawili (Plaster na Skimming) kwa kutumia White Cement?

Josh the best

New Member
Joined
Apr 22, 2019
Posts
2
Reaction score
0
Naombeni msaada wa ujenzi, eti unaweza kupiga plasta kwenye ukuta kwa kutumia white cement na ikawa umepiga ndege wawili kwa wakati mmoja yaani gharama za plasta ya kawaida na ya ku-skim baadae?
 
Hilo haliwezekani white cement haiwez tumika kwny plaster maana ina magnesium na iron iliongezwa kwa wingi ndo maana inakuwa nyeupe ambayo haiwezi kuchanganyika na mchanga kirahisi kwa kupiga na iko adhesive mnoo(ina hali ya ugundi zaidi) kuliko cement ya kawaida.

Kinachoweza kutumika ni cement ya kawaida inaweza changanywa na rangi na kutumika kuskimia lakini si white cement kwny plaster.
 
Naombeni msaada wa ujenzi eti unaweza piga plasta kwenye kuta kwa kutumia white cement na ikawa umepiga ndege wawili kwa wakati mmoja yaani gharama za plasta ya kawaida na ya ku skim baadae
Mkuu pia plaster huwa inafanya nyumba ipumue ukitumia white cement kwa ndani nyumba haiwezi kupumua.
 
Naombeni msaada wa ujenzi eti unaweza piga plasta kwenye kuta kwa kutumia white cement na ikawa umepiga ndege wawili kwa wakati mmoja yaani gharama za plasta ya kawaida na ya ku skim baadae.
Sasa hivi kuna njia nyingine inatumika na unapata matokeo yaleyale, lakini plasta lazima iwe imefanyika kwanza.

Mimi nilishauriwa kuchanganya cement na rangi na ukaskim kuliko kusikim kwa kutumia white cement, kumbuka mfuko wa cement ni shilingi 13000 mpaka 14000 wakati white cement ni elfu 18
 
Nimeskim saruji ya kawaida nikachangaya na rangi imetoka vizuri tu bila tatizo lolote

Na pia kama mchangajaji atatumia kipimo kimoja katila kuchangaya baso unapata kitu kimoja safi sana na hutajitaji rangi tena

Unapata rangi ya kijivu jivu nzuri tu
 
Naombeni msaada wa ujenzi, eti unaweza kupiga plasta kwenye ukuta kwa kutumia white cement na ikawa umepiga ndege wawili kwa wakati mmoja yaani gharama za plasta ya kawaida na ya ku-skim baadae?
White cement ipo juu kidogo usitumie kwenye plastaitakuala pesa nyingi, kwenye plasta tumia cement za kawaida , bali white cement uje kutumia kwenye skimming tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na bei ya rangi mbona hujahesabia?
Sasa hivi kuna njia nyingine inatumika na unapata matokeo yaleyale, lakini plasta lazima iwe imefanyika kwanza.

Mimi nilishauriwa kuchanganya cement na rangi na ukaskim kuliko kusikim kwa kutumia white cement, kumbuka mfuko wa cement ni shilingi 13000 mpaka 14000 wakati white cement ni elfu 18
 
Hilo haliwezekani white cement haiwez tumika kwny plaster maana ina magnesium na iron iliongezwa kwa wingi ndo maana inakuwa nyeupe ambayo haiwezi kuchanganyika na mchanga kirahisi kwa kupiga na iko adhesive mnoo(ina hali ya ugundi zaidi) kuliko cement ya kawaida.

Kinachoweza kutumika ni cement ya kawaida inaweza changanywa na rangi na kutumika kuskimia lakini si white cement kwny plaster.
mkuu, je wall plaster/sealer inaweza kutumika kama mbadala wa white cement au gypsum powder?
 
Piga plaster na cement za kawaida, baade kwenye skimming tumia white cement kwa nje na kama unataka kutumia powder ndani sio mbaya hutaona mipasuko wala fungas, nje ni ni lazima utumie white cement kwaajili ya weather
 
Piga plaster na cement za kawaida, baade kwenye skimming tumia white cement na gybroc powder hutaona mipasuko wala fungas
Mkuu plaster tiyari ndio nataka kufanya skimming. sasa ndio nilikuwa naomba kufaham skimming ya gypsum powder au white cement na wall plaster ni ipi nzuri na imara zaidi
 
Tumia white cement ni bomba zaidi
,

Mimi nilitumia white cement nje kote ndani nikatumia powder,ila ningejua ningepiga white cement ndani na nje inakua safi sana
 
Mkuu plaster tiyari ndio nataka kufanya skimming. sasa ndio nilikuwa naomba kufaham skimming ya gypsum powder au white cement na wall plaster ni ipi nzuri na imara zaidi
Hapa ni dinning ila ukuta wa bafuni pamoja kuna tiles ila inavyonza maji inaharibu ukuta wa dinning ingekua nimepiga ndani white cement hili lisingetokea,
IMG_20200712_164927.jpg
 
Ukipata fundi mzuri wa plaster huna haja ya skimming ....ukimaliza plaster unapiga emulsion nyeupe then unapiga rangi unayotaka.
 
Back
Top Bottom