Kwa mfano Kama Nilikuwa mlevi sana wa pombe kali na mvuta sigara kwa zaidi ya miaka 20 Sasa nikataka kujua hali yangu ya organ za ndani zipoje; yaani nijue kama kuna dalili za kansa ya mapafu,ini na Koo na pia nifanye kipimo Cha magonjwa ya Figo.
Je, hiyo check-up ya mwili hufanywa kwa vipimo gani mashine ipi na je hospital za hadhi gani?
Nina Bima ya afya NHIF so nielekezwe nafanyaje au namwombaje daktari ili akubali kunipima hata kama siumwi dalili zozote?
Vipimo vya kansa mwilini vyaweza kufanyika kwa kutegemea na athari ya kansa husika kwenye mwili. Mfano: kuongezeka kwa uvimbe/size huweza kuleta maumivu ambayo huweza kuwa dalili inayomleta mgonjwa hospitali. mfano: kansa ya ziwa, kuongezeka kwa vichocheo/hormone mfano: bhcg kwenye ujauzito ulioshindwa kuendelea kukua kwa makosa ya ki-jenetiki, PSA kwenye kansa kwenye tezi dume.
Hivyo unaweza kuanza kupima kulingana na chanzo na dalili:
1: Uvimbe (Xray/CT scan, Echomammography na MRI)
2: Vidonda na uvimbe (biopy)
3: Matezi (kupima kemikali husika/ ultrasound/biopsy)
4: Kemikali zinazopatikana mwilini kutokana na uwepo wa aina fulani ya kansa (tumor markers).
5: Kuchukua ulojo kwenye maeneo kama kakikati ya mifupa.
6: Nuclear medicine: sifa za uwezo wa kuchukua baadhi ya madini mwilini.
7: Multi-cancer DNA screening test/artificial intelligence. From blood biopsy
8: Kucheki figo, hii haina shida sana maana ni vipimo kama viatu kulingana na hali yako(Creatinine, Urea na Ultrasound). Labda kama kutakuwa na shida yoyote.
Kila kipimo hapo kina umuhimu kulingana na asili ya tatizo/kansa na ni kwa kiasi gani tatizo lilivyo.
Hivyo, upime nini kwenye check up hutegemea ni nini unataka kutokana na nini kufikia kama mwafaka. Mfano: kulingana na asili ya kazi, umri, jinsia na historia nyingine vyaweza kuwa na nafasi ya mtoa huduma aseme afanye nini kama vipimo baseline na non invasive/visivyo na madhira makubwa kwako kulingana na umuhimu.
NB: Kama ulivyoelezwa kuwa bima hazilipii check up. Inabidi kujua jinsi ya kucheza huu mdundo.