Msaada: Nawezaje kuziba matundu kwenye bati zilizowahi kutumika ili niezekee kwenye nyumba nyingine?

Msaada: Nawezaje kuziba matundu kwenye bati zilizowahi kutumika ili niezekee kwenye nyumba nyingine?

Last KING Ontuzu

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
644
Reaction score
927
Habari zenu wana jf,kutokana na bomoabomoa zinazoendelea kupisha ujenzi wa barabara nimejikuta naambulia bati na vitu vingine kama milango na madirisha.

Ninawaza kutumia bati zilezile pamoja na baadhi ya mbao,ili niezekee nyumba mpya kupunguza gharama za ujenzi ,bati ni za geji 28

Ni kwa namna gani naweza kuzuia bati hizo kuvuja wakati wa mvua?
 
nenda duka lolote la vifaa vya ujenzi watakupa gundi fulani hivi ipo kawa dawa ya meno ila ni nyeusi,utaiweka kwenye matundu ya bati lako,pia hii hutumika kubandikia vioo kwenye madirisha,nimesahau jina kwa sababu mara ya mwisho niliiona mwaka 2007
Mkuu Unamàñisha silicon au? Hata mimi ningemshauri atumie silicon nirahisi na very flexible
 
Yap mkuu inanata nata iko safi sana aende hardaware yeyote hatakosa

Basi ni hiyo mkuu,ipo vizuri sana japo sijaiona miaka mingi sana lakini unajua hapa nchini kwetu vitu vya miaka ya zamani sasa hivi hakuna mfano juzi nimetafuta sana antenna ya Tv zile za kuweka ndani nimekosa
 
basi ni hiyo mkuu,ipo vizuri sana japo sijaiona miaka mingi sana lakini unajua hapa nchini kwetu vitu vya miaka ya zamani sasa hivi hakuna mfano juzi nimetafuta sana antenna ya Tv zile za kuweka ndani nimekosa
Technolojia inatupeleka kasi sana .....nimeziona kwa wamachinga sana
 
Maduka yote ya Hardware na hasa wauzaji wa mabati wanazo dawa za kuzibia na hata silicon ni moja wapo zunguka apo Moshi utapata
ila usilogwe ukanunua Tinner haihusiki

Hapo nilikuwa nazungumzia antenna ya Tv mkuu,jamaa wa bati ni mwingine
 
Maduka yote ya Hardware na hasa wauzaji wa mabati wanazo dawa za kuzibia na hata silicon ni moja wapo zunguka apo Moshi utapata
ila usilogwe ukanunua Tinner haihusiki
Kwani Tinner ina matumizi gani mkuu!
 
Back
Top Bottom