Gundi kwa ajiri ya Bati Zipo aina nyingi ikitofautiana matumizi!
Kama ni Matundu ya Bati yaliyotokana na Misumari, kwa kawaida Msumari hugongwa kwenye Mgongo, hivyo kama Matundu yakiwa juu ya Mgongo ni ngumu Bati kuvuja... But ikibidi ndo unaweza kutumia Gundi!
Gundi ya Moto ni Bora kuliko Silicone inapokuja kuziba Matundu, Ila Gundi ya Moto na Silicone ni Bora zaidi Kama Bati linavuja pale Msumari ulipopigwa, Binafsi napendekeza Gundi ya Moto kwa sababu kadri inavyoanza kukauka Huwa inavimba hivyo kujaa kwenye Tundu!
Kama ni kuziba Tundu ambalo lipo wazi, Tumia Gundi ya Rami kwa ajiri ya Mabati, hii unaziba Matundu yaliyowazi kwa usahihi, na Kama Tundu ni kubwa unaweza kuchomeka Pamba kidogo then kwa juu ukasiriba na Gundi hiyo.
Bei ya Gundi zote ni kati ya 5,000 mpaka 10,000, haizidi 10,000.