Msaada ndoto zinanifanya na kuwa hofu

Mengi wamekushauri, na wengine wamekupa hata mistari ya neno la Mungu. Yote sawa ila namalizia hivi. Ndoto ya kweli ikija kwako, jua kuwa hilo jambo tiyari Mungu kishalishinda.
Mungu hufanya kazi pamoja na watu, haswa wale wampendao. Akikuonesha mtu flani amekufa, hakikisha kuwa unasimama imara na kuikemea hiyo roho ya mauti kwani umeoneshwa umwokoe huyo mtu. Ukiikemea hiyo roho itamwacha hivyo huna haja ya kwenda kumwambia.
Kama ukiota mtu flan anapata ajali, ni Mungu amekuonesha ili ukemee na pia unaweza kwenda kwake, muulize ka amepanga safari akisema ndiyo mwulize umuhimu wa safari hiyo. Kukiwa hakuna ulazima, mwambiye aache kwani umeota vibaya. Akienda na kuipata atakumbuka kuwa ulimwonya.
Kumbuka, nabii hakusi heshima isipokuwa kwa watu wa nyumbani mwake. Wakikudharau si weye umedharauliwa ila aliyekuonesha na kukutuma.
 
Unasali wapi?
...Hata Yusuf aliota ndoto...na kisa hiki ...kibo kwa wote Islam na Christian
 
Ubarikiwe sana kiongozi hakika nimepata kitu kutokana kukotoka kwenu, nitayafanyia kaz
 
Asante kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi
 
Mkuu shida inakuja pale nipoota kuna kifo kitatokea ktk familia na kweli baada ya siku kadhaa anaondoka mzazi, au kaka, mjomba nk, hapa tu ndo panifanya nikose aman,

Hizo ndoto azitoki kwa Mungu ila zinatoka kwa shetani hivyo cha kufanya soma biblia na omba asubuhi, usiku na kila wakati unapokuwa na muda. Hizo nguvu za shetani zitakukimbia
 
Ukiota mtu anakufa, msaidie kwenda kanisani kurekebisha mahusiano yake na Mungu; ili atakapokufa basi apumzike kwa amani. Ukiota mtu atapata hasara, mwambie afanye hata saving bank ili imsaidie kwenye rainy days
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…