Msaada ndoto zinanifanya na kuwa hofu

Msaada ndoto zinanifanya na kuwa hofu

Mengi wamekushauri, na wengine wamekupa hata mistari ya neno la Mungu. Yote sawa ila namalizia hivi. Ndoto ya kweli ikija kwako, jua kuwa hilo jambo tiyari Mungu kishalishinda.
Mungu hufanya kazi pamoja na watu, haswa wale wampendao. Akikuonesha mtu flani amekufa, hakikisha kuwa unasimama imara na kuikemea hiyo roho ya mauti kwani umeoneshwa umwokoe huyo mtu. Ukiikemea hiyo roho itamwacha hivyo huna haja ya kwenda kumwambia.
Kama ukiota mtu flan anapata ajali, ni Mungu amekuonesha ili ukemee na pia unaweza kwenda kwake, muulize ka amepanga safari akisema ndiyo mwulize umuhimu wa safari hiyo. Kukiwa hakuna ulazima, mwambiye aache kwani umeota vibaya. Akienda na kuipata atakumbuka kuwa ulimwonya.
Kumbuka, nabii hakusi heshima isipokuwa kwa watu wa nyumbani mwake. Wakikudharau si weye umedharauliwa ila aliyekuonesha na kukutuma.
 
Heshima kwenu mabibi na mabwana, bila kupoteza muda km mada tajwa hapo juu inavyosomeka ni kwamba, Mara nyingi nimekuwa nikiota ndoto baada ya muda kuna tukio lina tokea japokuwa huwa siletewi picha moja kwa moja ila mazingira ya ndoto na baada ya tukio halisi kutokea ndipo hupata picha kamili.

Ukweli sipendi hii hali kwani imenijengea hofu na woga mwingi, kwa Mara nyingine tena wwkati nimelala usiku wa kuamkia leo nilipata kuota ndoto, niliposhtuka sikupata tena usingizi hata kulipokucha, nilijiuliza maana yake nn ile ndoto lkn sikupata majibu, nikaishia kujifariji tu nakuendelea na shughuli zangu, ilipofika mchana nilipata simu toka kwa ndg yangu mmoja kuwa anatatizo, kwa vile sikuwa mbali na alipo nilimwambia anisubir, kufika pale hali mazingira niliyomkuta nayo na maneno aliyokuwa akinambia tayari nikaikumbuka ndoto niliyoota usiku, sitaki kusema kwa undani sana,

Nifanyeje nisiwe naota, kwani nimekuwa nikiota misiba na kweli inatokeA, au kuna MTU ataumwa na inakuwa, sipendi hii hali inanifanya nakuwa ktk mazingira magumu,
Unasali wapi?
...Hata Yusuf aliota ndoto...na kisa hiki ...kibo kwa wote Islam na Christian
 
Mengi wamekushauri, na wengine wamekupa hata mistari ya neno la Mungu. Yote sawa ila namalizia hivi. Ndoto ya kweli ikija kwako, jua kuwa hilo jambo tiyari Mungu kishalishinda.
Mungu hufanya kazi pamoja na watu, haswa wale wampendao. Akikuonesha mtu flani amekufa, hakikisha kuwa unasimama imara na kuikemea hiyo roho ya mauti kwani umeoneshwa umwokoe huyo mtu. Ukiikemea hiyo roho itamwacha hivyo huna haja ya kwenda kumwambia.
Kama ukiota mtu flan anapata ajali, ni Mungu amekuonesha ili ukemee na pia unaweza kwenda kwake, muulize ka amepanga safari akisema ndiyo mwulize umuhimu wa safari hiyo. Kukiwa hakuna ulazima, mwambiye aache kwani umeota vibaya. Akienda na kuipata atakumbuka kuwa ulimwonya.
Kumbuka, nabii hakusi heshima isipokuwa kwa watu wa nyumbani mwake. Wakikudharau si weye umedharauliwa ila aliyekuonesha na kukutuma.
Ubarikiwe sana kiongozi hakika nimepata kitu kutokana kukotoka kwenu, nitayafanyia kaz
 
Hupendi kuota???na ilihali yote unayoota yana ukweli ndani yake, labda hujakua na huelewi maana ya ndoto nakushauri kabla hujaaribu nyota yako tafuta mzee wa busara ambaye una uhakika ni mwelewa ila asiwe mchawi atakufundisha mengi kuhusiana na elimu ya unajimu
Asante kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi
 
Mkuu shida inakuja pale nipoota kuna kifo kitatokea ktk familia na kweli baada ya siku kadhaa anaondoka mzazi, au kaka, mjomba nk, hapa tu ndo panifanya nikose aman,

Hizo ndoto azitoki kwa Mungu ila zinatoka kwa shetani hivyo cha kufanya soma biblia na omba asubuhi, usiku na kila wakati unapokuwa na muda. Hizo nguvu za shetani zitakukimbia
 
Ukiota mtu anakufa, msaidie kwenda kanisani kurekebisha mahusiano yake na Mungu; ili atakapokufa basi apumzike kwa amani. Ukiota mtu atapata hasara, mwambie afanye hata saving bank ili imsaidie kwenye rainy days
 
Back
Top Bottom