Msaada ndugu yangu anakoweza kupata tiba ya ugonjwa unaomsumbua kwa muda mrefu

Moaz

Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
88
Reaction score
127
Habari Wakuu
Ninaomba msaada wa kupata daktari wa Jadi ambaye anaweza kumsaidia ndg yangu ambaye kwasasa ni kama amekata tamaa kabisa kutokana na kuhangaika pasina kufanikiwa. Historia yake fupi.

Amefanikiwa kuoa mke ambaye kabla ya mafanikio walikuwa na upendo tu mzuri na maelewano na hivo kufanikiwa kupata watoto ambao waliwalea vizuri na kipindi chote hicho ndg yangu ndio alikuwa ni kila kitu katika familia ghafla akaanza kuwa mgonjwa na kushindwa kutimiza baadhi ya majukumu na hivo ikamlazimu Mkewe aanze kufanya kazi ili kusupport baadhi ya majukumu na hapo ndipo Matatizo yakaanza.

Mke akawa anafanya atakalo watoto wakawa hawamsikilizi Baba yao na yeye hali ikazidi kuwa mbaya kiasi amekuwa kama mtu ambaye ametengwa mbaya zaidi Mke amefikia hatua anakuja na Watu nyumbani na wakionesha mahaba mazito ndugu yangu akiwa hana la kufanya na wala kauli. Na akiwasikia wakitamka wazi kuwa hawezi kupona kwa kuwa Magonjwa aliyo nayo sio ya kutibika Hospitalini na wala hakuna mtu yeyeto yule anayeweza kumtibu katika Dunia hii.

Ni miaka sasa amejaribu kupambana lakni ameshindwa kupata msaada na imefikia hatua ameshaanza kukata tamaa hata ya kupona.

Ombi langu ni kuwa hatujui nini amefanya ima yupo sahihi au yeye ndio chanzo anachoomba yeye ni kupata misaada wa ufumbuzi wa matatizo haya yanayomkabili kama kutakuwa na Mtu ambaye anafahamu mahala popote kule Nchini ambapo anaweza kupata Msaada tutashukuru kwa hilo.

Asanteni
 
Anasumbuliwa na nini? hujaweka wazi ni changamoto gani ya kiafya aliyo nayo
 
Anaumwa Kisukari, Pressure iko juu, kutokuelewa na familia mke na watoto kiufupi ana matatizo ya kiafya na kifamilia na yamefika katika hali mbaya ya kuweza mtu kukata tamaa Kiongozi
 
Pole sana. Lakini haya maradhi dawa za hosp zinasaidia pia.
 
Kiukweli dawa za hospitali ametumia sana kiasi hakuna kinachomsaidia na sio za hospitali hata baadhi za kienyeji nazo ametumia lkn hali bado haijatengamaa ndio maana anahisia maybe inaweza ikawa kuna Uswahili maana nae alikuwa sio mtu wa kuamini mambo ya kiswahili
 
Polen sana,,,, ! Mke kama vile anachekelea ugonjwa wa jamaa , na alikula kiapo wataishi kwa shida na raha mpaka kifo kiwatenganishe, so sad
 
Daah nimesikitika sana kwa hii story aise mnakukata sana moto vijana tuotaka kuoa. Nimeshangaa sijaona reply ya wale jamaa wa KATAA NDOA. Mwisho, Mungu atamsaidia arudi kwenye hali yake ya kawaida
 
Shukran Kaka Ndoa zina mambo mengi sana
 
Huyo mwanaume anaacha kudili na ugonjwa wake naona yuko kufatilia matendo ya mkewe…!!
Km ana sukari inamaanisha hata jogoo haliwiki, sasa hapo lazima mke wasielewane..!!

Hata ingekuwa yeye lazima angetafuta pa kumalizia hamu zake… aache lawama.

Kuhusu kurogwa sina uhakika, km ugonjwa ushaonekana hospital hapo yeye kufata ushauri wa wataalamu na kunywa dawa..!! Gubu halitomsaidia aangalie afya yake kwanza..!!
 
Sawa ametumia dawa za hospital, je anafuata masharti ya vyakula? Maana ni bure Kama utameza dawa za pressure bila kushughulika na cholesterol Kama ipo juu.
Pia ni bure Kama utameza au kuchoma insulin bila kufuata masharti ya chakula kwa wenye kisukari.

Nakushauri nenda hospital kubwa na mtakachoambiwa afuate kwa uhakika masharti anayopewa.
 
Mimi ninesoma uzi hapajatwa tatizo lake hasa linalomsumbua.
 
Anaumwa aina gani ya ugonjwa ?

Na je nyie ndugu zake kwanini msimchukue na mkaishi nae na kumuhudumia Kwa njia tofauti ,tofauti.

Na je kwakuwa ndugu yenu yupo na Changamoto Kama Hiyo je kwanini msichukue jukumu la kulea watoto wake?

Kama nyie ni ndugu zake jaribuni kuwa responsible kwanza then mkifika hatua ambayo hamuwezi muombe msaada.

Ikiwa mwanamke amekuwa breadwinners - hii ni kawaida Kwa wanawake wakibantu asilimia kubwa wamelelewa na kufunzwa wao hawausiki na kuleta mkate wao ni kuzaa na kulea tu.

Pia swala la kuleta wanaume anapoishi Mme wake , hii Ana fan ya makusudi kumfanyia Psychological torture. Kitu ambacho anashindwa kutazama mbele

So sifikirii Kama ndoa ni Kwa ajili ya sex kwamba mmoja wenu akiumwa akashindwa kufanya sex basi mnabidi kuachana na Kama ndo hivi hamna umuhimu wa hilo jambo la kuishi na Mwanamke , Mwanamke au mwanaume anabidi kukaa katika role ya partner.
 
Anaumwa Kisukari, Pressure iko juu, kutokuelewa na familia mke na watoto kiufupi ana matatizo ya kiafya na kifamilia na yamefika katika hali mbaya ya kuweza mtu kukata tamaa Kiongozi
poleni sana, hapo apambane tuu na hospital achaneni na waganga, kuhusu mke analeta dharau kwakuwa mume wake awezi kazi tena, ila hujafa hujaumbika atalipwa hapa hapa duniani.
 
Habari Wakuu
Ninaomba msaada wa kupata daktari wa Jadi ambaye anaweza kumsaidia ndg yangu ambaye kwasasa ni kama amekata tamaa kabisa kutokana na kuhangaika pasina kufanikiwa. Historia yake fupi.

Amefanikiwa kuoa mke ambaye kabla ya mafanikio walikuwa na upendo tu mzuri na maelewano na hivo kufanikiwa kupata watoto ambao waliwalea vizuri na kipindi chote hicho ndg yangu ndio alikuwa ni kila kitu katika familia ghafla akaanza kuwa mgonjwa na kushindwa kutimiza baadhi ya majukumu na hivo ikamlazimu Mkewe aanze kufanya kazi ili kusupport baadhi ya majukumu na hapo ndipo Matatizo yakaanza.

Mke akawa anafanya atakalo watoto wakawa hawamsikilizi Baba yao na yeye hali ikazidi kuwa mbaya kiasi amekuwa kama mtu ambaye ametengwa mbaya zaidi Mke amefikia hatua anakuja na Watu nyumbani na wakionesha mahaba mazito ndugu yangu akiwa hana la kufanya na wala kauli. Na akiwasikia wakitamka wazi kuwa hawezi kupona kwa kuwa Magonjwa aliyo nayo sio ya kutibika Hospitalini na wala hakuna mtu yeyeto yule anayeweza kumtibu katika Dunia hii.

Ni miaka sasa amejaribu kupambana lakni ameshindwa kupata msaada na imefikia hatua ameshaanza kukata tamaa hata ya kupona.

Ombi langu ni kuwa hatujui nini amefanya ima yupo sahihi au yeye ndio chanzo anachoomba yeye ni kupata misaada wa ufumbuzi wa matatizo haya yanayomkabili kama kutakuwa na Mtu ambaye anafahamu mahala popote kule Nchini ambapo anaweza kupata Msaada tutashukuru kwa hilo.

Asanteni
Hujasema tatizo gani
 
Anaumwa Kisukari, Pressure iko juu, kutokuelewa na familia mke na watoto kiufupi ana matatizo ya kiafya na kifamilia na yamefika katika hali mbaya ya kuweza mtu kukata tamaa Kiongozi
hapo issue ni depression ( msongo wa mawazo) itapendeza z!aidi kama wataalamu wa afya ya akili watahusishwa. Nitarudi
 
Back
Top Bottom