Msaada ndugu yangu anakoweza kupata tiba ya ugonjwa unaomsumbua kwa muda mrefu

Msaada ndugu yangu anakoweza kupata tiba ya ugonjwa unaomsumbua kwa muda mrefu

Mchukueni mrudisheni kwao , mtakuja kupata tabu kusafirisha maiti . Hivyo vimbwanga anavyofanyiwa na mkewe hasa kuchepuka vinamuathiri sana kisaikolojia.
 
Sawa ametumia dawa za hospital, je anafuata masharti ya vyakula? Maana ni bure Kama utameza dawa za pressure bila kushughulika na cholesterol Kama ipo juu.
Pia ni bure Kama utameza au kuchoma insulin bila kufuata masharti ya chakula kwa wenye kisukari.

Nakushauri nenda hospital kubwa na mtakachoambiwa afuate kwa uhakika masharti anayopewa.
Shukran kiongozi kwa Mawazo yako but tusharibu hospitali kubwa na imekuwa very complicated mpaka wataalamu wanashindwa kuelewa kwasababu hakuna majibu ya kueleweka
 
Hata nyie pia kuna time mnazingua msitoe lawama kwa wanawake tu..
Huyo mwanaume anaacha kudili na ugonjwa wake naona yuko kufatilia matendo ya mkewe…!!
Km ana sukari inamaanisha hata jogoo haliwiki, sasa hapo lazima mke wasielewane..!!

Hata ingekuwa yeye lazima angetafuta pa kumalizia hamu zake… aache lawama.

Kuhusu kurogwa sina uhakika, km ugonjwa ushaonekana hospital hapo yeye kufata ushauri wa wataalamu na kunywa dawa..!! Gubu halitomsaidia aangalie afya yake kwanza..!!
Shukran kwa mawazo hakika tutayafanyia kazi
 
Pole sana mkuu dunia mapito japo sijaelewa tatizo kwa undani nichek pm
 
Habari Wakuu
Ninaomba msaada wa kupata daktari wa Jadi ambaye anaweza kumsaidia ndg yangu ambaye kwasasa ni kama amekata tamaa kabisa kutokana na kuhangaika pasina kufanikiwa. Historia yake fupi.

Amefanikiwa kuoa mke ambaye kabla ya mafanikio walikuwa na upendo tu mzuri na maelewano na hivo kufanikiwa kupata watoto ambao waliwalea vizuri na kipindi chote hicho ndg yangu ndio alikuwa ni kila kitu katika familia ghafla akaanza kuwa mgonjwa na kushindwa kutimiza baadhi ya majukumu na hivo ikamlazimu Mkewe aanze kufanya kazi ili kusupport baadhi ya majukumu na hapo ndipo Matatizo yakaanza.

Mke akawa anafanya atakalo watoto wakawa hawamsikilizi Baba yao na yeye hali ikazidi kuwa mbaya kiasi amekuwa kama mtu ambaye ametengwa mbaya zaidi Mke amefikia hatua anakuja na Watu nyumbani na wakionesha mahaba mazito ndugu yangu akiwa hana la kufanya na wala kauli. Na akiwasikia wakitamka wazi kuwa hawezi kupona kwa kuwa Magonjwa aliyo nayo sio ya kutibika Hospitalini na wala hakuna mtu yeyeto yule anayeweza kumtibu katika Dunia hii.

Ni miaka sasa amejaribu kupambana lakni ameshindwa kupata msaada na imefikia hatua ameshaanza kukata tamaa hata ya kupona.

Ombi langu ni kuwa hatujui nini amefanya ima yupo sahihi au yeye ndio chanzo anachoomba yeye ni kupata misaada wa ufumbuzi wa matatizo haya yanayomkabili kama kutakuwa na Mtu ambaye anafahamu mahala popote kule Nchini ambapo anaweza kupata Msaada tutashukuru kwa hilo.

Asanteni
Mkuu mgonjwa Umri wake miaka mingap
 
Shukran kiongozi kwa Mawazo yako but tusharibu hospitali kubwa na imekuwa very complicated mpaka wataalamu wanashindwa kuelewa kwasababu hakuna majibu ya kueleweka
Mkuu kwa magonjwa hayo unayoyataja wataalamu hawawezi kushindwa kuelewa. Ni labda hamfuati masharti au matumizi ya dawa hayazingatiwi.

Pressure na sukari ni magonjwa yanayohusiana kwa hivo usipo-control pressure sukari itasumbua and kinyume chake!
 
Mkuu kwa magonjwa hayo unayoyataja wataalamu hawawezi kushindwa kuelewa. Ni labda hamfuati masharti au matumizi ya dawa hayazingatiwi.

Pressure na sukari ni magonjwa yanayohusiana kwa hivo usipo-control pressure sukari itasumbua and kinyume chake!
Shukrani Kiongozi Kwa Ushauri wako tutaufanyia kazi
 
Back
Top Bottom