Msaada: Ndugu yangu ni dereva wa lori ana kesi ya kugonga (traffic case)

Msaada: Ndugu yangu ni dereva wa lori ana kesi ya kugonga (traffic case)

Jambo la msingi hakikisha ile familia ya mfiwa haina neno nanyi, usiseme wapo kimya tu lazima ujue kwa undani mioyo yao ipo safi!?

Baada ya hapo muone hakimu au askar anayehusika na hiyo kesi kujua muafaka.

Kukataa kesi ni ujinga akati kweli umefanya na ni suala la kawaida haya mambo.
Nimekuelewa mkuu
 
Poleni Sana Mwambie asiogope Hiyo traffic case inaenda mahakamani ataulizwa tu Kama ni kweli atajibu kwa kawaida kwa kua akukusudia inabidi alipe faini ambayo hua ni elfu 56000 Kama sijakosea na jalada hua linafungwa

Tafuta mwanasheria mpeni elfu 10 atawaelezea vizuri
Sawa tutafanya hivyo ndugu yangu
 
Kwanza Pole Kwa wafiwa, kama kesi Imeshafika kwa Pilato hamna namna.

Cha Kwanza Mambo ya Jembe lake liko huko huko achana nayo kbs, ujue hapo uhai wa mtu umetoka. usije kuwatibua wafiwa.
Hao Wafiwa kuwa Karibu nao ili huyo mwanasheria akiuliza unasema nimeshawaona na pole nimewapa!

Ukifanya hivyo unawarahisishia Kazi Mwendesha Mashtaka na Bw.Pilato. Kaa nao Vizuri Mwanasheria na Bw. Pilato, Sijui Ushanfahamu hapo.? haitakiwi kutoa detail sana kwenye ushauri. Mambo ya Akatae au Akubali watafundishana mbele kwa mbele.
Nashukuru sana mkuu wangu, nimepata mwongozo kwa hili
 
Back
Top Bottom