mwalidebe
JF-Expert Member
- Mar 27, 2016
- 425
- 250
Ndugu,jamaa,marafiki na members wote wa Jamii forums, naombeni msaada wenu wa ushauri na mawazo yenu. Kuna tatizo linanisumbua muda mrefu sasa kila ninapo maliza kuoga napatwa na muwasho wa ngozi mwili mzima,yaani mpaka huwa natamani nisioge je nini nifanye niondokane na tatizo hili? Binafsi kabla sijalileta kwenu nimeshatumia dawa mbalimbali kutoka maduka ya dawa zile za kupaka na za kumeza pia nimetumia sabuni za kuondoa muwasho Mara ya mwisho nilienda hospitali ya binafsi doctor alinipa ushauri na dawa moja ya kupaka
lakini mpaka sasa bado tatizo linaendelea je watanzania wenzangu nini nifanye? Muwasho huu ni kama vile aliyewai kutumia dawa ya kororokwini ndivyo ninavyowasha baada tu ya kumaliza kuoga ila baada ya dakika ishirini muwasho hupungua taratibu na mwili kurudi katika hali ya kawaida. Pia kama umewai kupitia tatizo hili nitashukuru ukiniambia jinsi ulivyokabiliana nalo.