Msaada ndugu zangu

Msaada ndugu zangu

mwalidebe

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2016
Posts
425
Reaction score
250
Ndugu,jamaa,marafiki na members wote wa Jamii forums, naombeni msaada wenu wa ushauri na mawazo yenu. Kuna tatizo linanisumbua muda mrefu sasa kila ninapo maliza kuoga napatwa na muwasho wa ngozi mwili mzima,yaani mpaka huwa natamani nisioge je nini nifanye niondokane na tatizo hili? Binafsi kabla sijalileta kwenu nimeshatumia dawa mbalimbali kutoka maduka ya dawa zile za kupaka na za kumeza pia nimetumia sabuni za kuondoa muwasho Mara ya mwisho nilienda hospitali ya binafsi doctor alinipa ushauri na dawa moja ya kupaka
bf61978f3bc13ae1bc989b45ea14a24a.jpg
lakini mpaka sasa bado tatizo linaendelea je watanzania wenzangu nini nifanye? Muwasho huu ni kama vile aliyewai kutumia dawa ya kororokwini ndivyo ninavyowasha baada tu ya kumaliza kuoga ila baada ya dakika ishirini muwasho hupungua taratibu na mwili kurudi katika hali ya kawaida. Pia kama umewai kupitia tatizo hili nitashukuru ukiniambia jinsi ulivyokabiliana nalo.
 
Pole sana, madaktari hawakuwahi kukuelezea chanzo kuwa ni kitu gani.
Hebu check ujue sababu itakuwa moja kati njia za kulitatua tatizo ..

Pia ungeeleza hilo tatizo lina muda gani kwenye mwili wako..

Je ushawahi kuogelea baharini, na he hali ilikuwa sawa na unavyooga?/ au ukinawa hali inakuwaje.

Je ni sehemu gani za mwili huwasha zaidi, miguuni, au mikononi au shingoni au kichwani?

Kumbuka ukimweleza daktari tatizo lako kwa kina, kulingana na historia ya tatizo, anaweza kutambua na kukupa tiba sahihi.. pole mkuu watakuja madaktari wakupe ushauri.
 
Kama una kunywa pombe acha kabisa. ..pole sana
 
Uki Google itakuelewesha vizuri. .
 
mimi nikiogea sabuni ya ukwaju nawashwa balaa
Haikufai hiyo


Ila serious.kuna makala.nilisomaga zamani kuna mtu alikuwa na mzio na maji...akioga tu ni ngwaraaa ngwaraaaa ngwaraaa ngwaraaaa...full kujikuna
 
Maybe sabuni unayotumia kuogea.
 
KWANZA acha uchafu, angalia huo mdafutari ulivyo mchafu, pamba za kusafisha masikio zilizotumika umeweka hovyohovyo tu, wewe utakuwa hata taulo hufui.
 
Mkuu achana na masuala ya kuoga oga we ule. Muda wa kuoga fanya vitu vingine
 
Niliwahi kuwa na tatizo hilo wakati nipo secondary, ilikuwa kwangu kuoga ni kama adhabu. Nilitumia sabuni na dawa mbali mbali bila mafanikio. Mwisho wa siku nilishauriwa yafuatayo:-
1. Kuoga maji ya uvuguvugu kwa siku za mwanzo huku ukihakikisha unatakata vizuri sana
2. Oga kwa kufuata muda maalumu, mimi nilikuwa naogo kila siku asubuhi (Jaribu kufuatilia muda kwa kipindi fulani)
3. Fua na kausha taulo vizuri (lisivundie chumbani), au jitahidi maji yakauke yenyewe mwilini bila taulo
4.Tumia mafuta ambayo yataifanya ngozi yako iwe laini, unapokuwa na tatizo hili mara nyingi ngozi yako inakuwa kavu na hupauka haraka baada ya kuoga.

Nilifanya hivyo, na baada ya muda nilianza kufurahia kuoga. Kwa sasa sifuati tena muda maalumu wa kuoga, ila mengine ni sehemuu ya maisha yangu

Hope itasaidia
 
KWANZA acha uchafu, angalia huo mdafutari ulivyo mchafu, pamba za kusafisha masikio zilizotumika umeweka hovyohovyo tu, wewe utakuwa hata taulo hufui.
Yaani wewe mchokonoko sana umevumbua hata visivyo husika!!!
 
Hiyo fungus bro. Cha kufanya onana na daktari bingwa utapata matibabu sahihi
 
Back
Top Bottom