Msaada: Nguruwe wanakataa kula chakula

Kama unakiri kuna mahidi mabovu, sidhani kama kuna mchawi hapo, badilisha chakula.
Alafu mifugo mnailisha sumu kuvu, bila kujua ya kuwa itakuja kuhamia kwa Binaadamu kupitia kula nyama yao.
 
Mi najuwa Nguruwe anakula mpaka Mavi,Sasa kama msosi kaushindwa nguruwe basi utakuwa ndaza.
 
unajua nini mkuu..hii Jf siku hizi napita mara chache tofauti na miaka hio kurudi nyuma..siku hizi yeyote ata asiyejua thamani ya bando anacoment hata hakifahamu anacomment..zamani ulikua ukichangia watu wanadai tupe data(facts) adi ilikuwa raha ulikuwa huna haja ya kujiunga sosial media nyingine nondo zilikuwa zinashuka hapa siku hizi naona umekuwa mtaro wa maji taka...zote zimo.
 
Ugonjwa mbaya huo huku makambako wametakiwa kuwaua kwa hiari hao nguruwe au kuuliwa na maafisa mifugo. Wanaanza hvyo mwishoni wanakufa.

Note me.
 
Kabisa mkuu, kila mtu anapenda utani na mzaha japokuwa huku tunakuja kujifunza uzaha na matani tunayapeleka MMU na chit chat huko, mji bila wazee haukaliki.
 
Member since 8/8/2015
Nilijua mkongwe humu

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida iko wapi kuwa member toka 2015? Kumbuka ili uweze kucomment JF ni lazima u-log in au la hujajiunga basi una Register account yako. What if alikuwa anaangalia michango toka 2014 lakini akajiunga 2015? Point is jamaa kaja na tatizo critical watu badala ya kumsaidia wanaanza kuandika jokes na wakati hawajampa solution. Ukisoma comment ya jamaa tayari ashakata tamaa anataka kuuza mifugo wake kisa hajapata ushauri wa kitaalamu.
 
Habari Mkuu Pole kwa yaliyokukuta.

Naomba kutoa maelezo kidogo ambayo yanaweza yakawa msaada kwako na kwa wengine:

Kwanza Mahindi yaliyoharibika kutafanya kuwa chakula cha nguruwe wako sio jambo zuri na kama nguruwe wako wangefanikiwa kula uwezekano wa kupata magonjwa yatokanayo na fangasi (Fungal diseases) ungekuwa mkubwa vilevile sumu inayozalishwa na fangasi ingeathiri pia nguruwe wako na kupelekea vifo.

Chakula cha nafaka au pumba zisipo hifadhiwa vizuri au zikiwa na unyevunyevu au hata kuhifadhiwa kwa mda mrefu hutengeneza Fangasi (Fungus) mara nyingi huwa ni Mould chapo zipo aina nyingi, na Fangasi hizi huwa na madhara kama nilivyoeleza hapo juu.

Kuhusu kuacha kula;
Hapo sababu zinaweza kuwa zaidi ya moja
Kwanza Aina ya chakula unachowapa, Taste ya chakula kama ulivyosema ni kibovu.
Pili magonjwa ambayo yanawanyima hamu ya kula nguruwe wako yanaweza yakawa magonjwa ya kizazi au Cancer kwenye mfumo wa chakula na mengine mengi.
Tatu nguruwe wako huenda wana "constipation" haja ngumu jaribu kuchunguza kinyesi chao ili ujue kama ni hilo tatizo ambalo huathiri mfumo wa chakula.

Ushauri wangu:
•Acha mara moja kuwapa hicho chakula kibovu na tafuta chakula kingine kinachofaa kwaajili ya nguruwe wako. Zingatia aina ya chakula unachowapa.
•Muone Tabibu au mtaalamu wa Mifugo ili aweze kukusaidia kujua tatizo kiundani kama ni magonjwa atakueleza na njia za kufuata
•Jaribu pia kuwapa Multivitamin ili kurudisha appetite/hamu ya chakula waweze kuendelea kula wakati unatafta mtaalam wa kukutibia.
Shukrani.
 
Pilipili inaleta ladha na hamu ya msosi chukua pilipili kichaa kama debe 8 kausha alafu saga tena na hayo makande watapiga msosi wote
 
Kwanza yawezekana nguruwe wako ana minyooo huwa inapelekea kutokula vizuri au chakula kina madhara kwake huwa anakikwepa kwa kutokula
 
Inawezekan watakuwa na minyoo kama hujawapatia dawa ya minyoo mda mrefu wachome ivermectin au wapatie pia na multivitamn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…