Habari Mkuu Pole kwa yaliyokukuta.
Naomba kutoa maelezo kidogo ambayo yanaweza yakawa msaada kwako na kwa wengine:
Kwanza Mahindi yaliyoharibika kutafanya kuwa chakula cha nguruwe wako sio jambo zuri na kama nguruwe wako wangefanikiwa kula uwezekano wa kupata magonjwa yatokanayo na fangasi (Fungal diseases) ungekuwa mkubwa vilevile sumu inayozalishwa na fangasi ingeathiri pia nguruwe wako na kupelekea vifo.
Chakula cha nafaka au pumba zisipo hifadhiwa vizuri au zikiwa na unyevunyevu au hata kuhifadhiwa kwa mda mrefu hutengeneza Fangasi (Fungus) mara nyingi huwa ni Mould chapo zipo aina nyingi, na Fangasi hizi huwa na madhara kama nilivyoeleza hapo juu.
Kuhusu kuacha kula;
Hapo sababu zinaweza kuwa zaidi ya moja
Kwanza Aina ya chakula unachowapa, Taste ya chakula kama ulivyosema ni kibovu.
Pili magonjwa ambayo yanawanyima hamu ya kula nguruwe wako yanaweza yakawa magonjwa ya kizazi au Cancer kwenye mfumo wa chakula na mengine mengi.
Tatu nguruwe wako huenda wana "constipation" haja ngumu jaribu kuchunguza kinyesi chao ili ujue kama ni hilo tatizo ambalo huathiri mfumo wa chakula.
Ushauri wangu:
•Acha mara moja kuwapa hicho chakula kibovu na tafuta chakula kingine kinachofaa kwaajili ya nguruwe wako. Zingatia aina ya chakula unachowapa.
•Muone Tabibu au mtaalamu wa Mifugo ili aweze kukusaidia kujua tatizo kiundani kama ni magonjwa atakueleza na njia za kufuata
•Jaribu pia kuwapa Multivitamin ili kurudisha appetite/hamu ya chakula waweze kuendelea kula wakati unatafta mtaalam wa kukutibia.
Shukrani.