Unachotakiwa kuwa nacho ni FTA Decoder ambazo hukamata channels za bure toka satellite mbalimbali zilizopo angani au unaweza pia kuwa na TV yenye decoder ndani ( Inbuilt decoder). Flat smart TV nyingi sasa hivi zina hicho kisimbuzi cha ndani ya tv, ila wachache huweza kung'amua.
Tafuta dish aidha ya prime focus/Ku-band (yanayotumiwa na kampuni za tv za malipo kama Azam, Dstv,Startimes, likiwa kubwa/Pana Ni vizuri zaidi) au yale ya offset. Kisha angalia uwepo wa mawimbi ya satellite yaliyopatikana katika eneo unaloishi. Kwa mfano Kanda ya ziwa, baadhi ya mikoa ya Katavi,Rukwa,Tabora,Kigoma,Shinyanga wanaweza kunasa kwa kutumia dish la cm 60 (yale ya Dstv au Azam saizi ya kati au kubwa)kupitia satellites za Astra 28.2 East ambazo mawimbi yake yanafika mikoa hiyo. Humo kuna tv za Joy prime na Adom wanaonyesha. Kule Nyanda za juu kusini wanaweza kukamata Eutelsat 16°.
Kwa elimu zaidi pitia huu uzi
Hapo katika dishi la c band hilo kubwa ni uelekeo wa Azerspsce degree 45 e hapo unapata Clouds tv, Star tv, Channel ten, tv E, Mwangaza na Wasafi tv bila malipo kwa mwezi. Hilo dishi la kushoto ni uelekeo wa Eutelsat 7 e (Azam tv) Ila ukilizongusha kidogo tu kurudi kushoto ukiwa umesimama mbele...