Msaada: Ni mambo gani ya kuzingatia ukiwa M.C wa hafla mbalimbali?

Msaada: Ni mambo gani ya kuzingatia ukiwa M.C wa hafla mbalimbali?

...karibu kwenye dili zenye kuingiza mshiko bila jasho.

...tafuta clips za MC's youtube uone namna wanvyoendesha shughuli.

...jaribu kucheck clips za watu kama MC Luvanda hivi.

...kuwa na maneno ya heshima, zingatia ratiba, chekesha watu inapobidi, jua tamaduni za uwaongozao, kuwa na DJ mnayejuana etc

Huyo Mmenye aliachaje kazi Stanbic na kuingia kwenye u-MC? Jamaa naona anakuja kwa kasi ana host hadi show za kina P-square.
 
Kuna shughuli moja Mc alikua mpoki jamani jamaa anajua nahisi ukiwa Mc ukatuni unatakiwa sana!
 
okey okey
nimegeee nipe na experience mbaya iliyowahi kukuta

Kama nakukumbuka vile! Ushakuja Tabora kwenye harusi ya E...... na K........ Mbona uko vizuri sana kuliko hata Mpoki! Ukija bongo utakuwa juu sana! Take it from me.
 
Mimi nitakuelewesha kutokana na ulivyo niuliza kwenye mada kuhusu kuwa M.Cs katika sherehe ya watu wa kisukuma.
kitu cha kwanza unatakiwa angalau uwe unajua maneno baadhi ya kisuma, au kujua lugha ya kisukuma.
tatu kuwa mtu unayependa kuchekesha, maana wasukuma tukiwa pamoja tunapenda kufarahia.
tatu, kuwa mtu anayejua na kupenda matani, na matani yawe sehemu ya maisha yako.
nine kujiamini ni swala muhumi sana.

ukizangatia hayo RAFIKI YANGU masai dada naami utaweza kusherehesha sherehe yoyote ya watu wa kisukuma. asante
 
Last edited by a moderator:

asante my best friend from shytown,...,,
 
Last edited by a moderator:
Huyo Mmenye aliachaje kazi Stanbic na kuingia kwenye u-MC? Jamaa naona anakuja kwa kasi ana host hadi show za kina P-square.

M.C inalioa sana ukiwa vizuri
maana piga idadi ya sherehe unazoudhuria hao unaokitana nao na wenyewe wanaenda kuwaambia watu
na hao watu wanaambie wemgine so ukiwa vyema basi una make money
 
Kama nakukumbuka vile! Ushakuja Tabora kwenye harusi ya E...... na K........ Mbona uko vizuri sana kuliko hata Mpoki! Ukija bongo utakuwa juu sana! Take it from me.

hahahah mkuuu unaniwazia mema sana
thanx
 
Mambo muhimu ya kuzingatia;

> Kufanya mazoezi kabla ya tukio husika(unaweza kuigiza ukiwa na marafiki au ndugu halafu unawauliza wanaonaje unachokifanya

> Kuwafahamu wahusika yaani kukutana na pande zote za wahusika ili kupata taarifa zao ambazo utazitumia wakati wa shughuli husika kwa mfano, kuwatambulisha wahusika maalum mbele ya wageni waalikwa.

> Kujua mfululizo wa matukio kwenye tukio husika, kwa mfano, muda wa kuingia/kuanza sherehe, muda wa kuwatambulisha wahusika, nyimbo zitakazopigwa kwa kufuata mpangilio(hapa utatakiwa kuongea na dj mapema), nyimbo zitakazokubalika kwa wahusika(sio taarab kwenye sherehe za kikristo, au kupiga nyimbo za akina rose muhando kwenye sherehe za waislam.

> Kuepuka kutamka maneno yanayoweza kuwafanya watu wajisikie vibaya, zungumza maneno yenye kufurahisha na kuchekesha.

> Vaa mavazi mazuri kulingana na tukio husika, mavazi ya staha ni muhimu.

> Kujiamini/jione Kuwa wewe unaweza na si kushindwa.

> Zingatia kwenda na muda, hapa utapatiwa script ya tukio zima na watu wa kamati ya harusi au hata birthday kisha na wewe unaweza kuandaa mwongozo wako kutegemea mwongozo (main script) utakayopewa, kama hakuna mwongozo basi unaweza kuutayarisha mwenyewe kwa kuwashirikisha wasimamizi wa tukio husika.

> Kuwashirikisha wageni waalikwa ili kuvuta usikivu wao na kuwafanya wajione nao ni wahusika muhimu; hapa utatakiwa kuandaa maswali ya kuwauliza wageni waalikwa kama vile......."..jamani bwana harusi amependeza au hajapendeza"? Ukishauliza utakaa kimya ili kusikia muitikio wao wa swali ulilowauliza.

> Ucheshi/uchangamfu.

ZINGATIA MUDA NA RATIBA.
 
Honestly hiyo kazi naona ngumu sana
binafsi naona unapaswa kuwa na talent nayo au uwe kauzu vya kutosha
but jaribu uone
huwezi jua kama una talent or not kama hutajaribu...

nafikiri unapaswa kujua wewe mwenyewe vitu gani vinakuboa ukienda kwenye sherrehe ili usivifanye

U-mc na ukauzu!!!!! Hapana.
 
Golden 45 Minutes...ukiwa beginner au mc ukiwa ktk hadhira mpya kabisa kwako zitumie vema dk 45 za mwanzo....ndani ya dk hizo hakikisha hadhira yako inakubali kwamba leo wana.mc....ukibug hapo wakikujaji juwa wewe sio utapata shida sherehe nzima
 
Ktk kolabo utakayopiga na jamaa msizungumze wote kwa wakati mmoja akupe vipande vyako pekee kama vi3...anza wewe na vipande vya mwanzo ambavyo kiasili vimepooza....kisha muachie aingize maharusi na kuendelea mpaka wakati wa keki na chakula chukua wewe...muache amalizie zawadi...maeneo anayoshika yeye muangalie kwa makini ujifunze yaliyo mazuri
 
Kuhusu matukio magumu kunitokea hata nikikuambia haitakusaidia as beginner...swala mama huwa anamfundisha mwanae kula majani wala hamuambii kama kuna simba porini maana akimuambia swala mtoto ataogopa kutoka kutafuta majani mwishoe atakufa njaa.asante all the best
 
Wadau naomba kujulishwa hii biashara!

Mwaka jana mwishoni nilipata wasaa wa kukutana na M.C mmoja wa maeneo ya Temeke akasema kwamba nina sauti yenye ujazo inayoweza kunipatia mpaka million moja kwa weekend moja, pia muonekano you know
Kwamba inafaa sana kwenye shughuli mbalimbali.

Sio M.C wa HipHop MO11, hapana, ni wa sherehe; Msema Chochote a.k.a MC!

Sasa kuna sherehe kama mbili hivi ndogo ndogo moja ni tarehe 20 nita Co-host nae aniangalie, lakini pia iwe moja ya mafunzo.

Kiukweli, Sikuwahi kuwa na interest na hii shughuli na hata birthday party sijawahi kuwa MC. Please naomba ABC kwa makabila mbalimbali yapi ya kusema mbinu za kufanya uwe best MC, ili nitengeneze Mia mbili Mia tatu!

Makabila kama ya washana mshana jr mpwa naomba msaada wako, bwana utafiti najua umepitia mengi hapa nitapata ABC, le big boss The Boss, Shyland nambie sherehe za Kisukuma nisije nika uponda udaga maana nimezoea nyama ikawa tatizo.

Please bwana Pasco najua uko busy ila mchango wako ni muhimu na wote wote please msaada tutani.

Changamkia fursa hiyo Dada, hakuna shughuli ya kutengeneza hela kiulaini hapa mjini kama hiyo. Unapiga domo tu kwa masaa kama 4 hivi unaondoka na kiasi cha chini 500,000/=. Hapo ni mwanzo, ukijenga jina likawa kubwa kama kina MC Luvanda, Piliplili, Kitunguu, Cheni, na wengine maarufu kwa wiki hukosi 3,000,000/=. Mungu akupe nini?
 
Mambo muhimu ya kuzingatia;

> Kufanya mazoezi kabla ya tukio husika(unaweza kuigiza ukiwa na marafiki au ndugu halafu unawauliza wanaonaje unachokifanya

> Kuwafahamu wahusika yaani kukutana na pande zote za wahusika ili kupata taarifa zao ambazo utazitumia wakati wa shughuli husika kwa mfano, kuwatambulisha wahusika maalum mbele ya wageni waalikwa.

> Kujua mfululizo wa matukio kwenye tukio husika, kwa mfano, muda wa kuingia/kuanza sherehe, muda wa kuwatambulisha wahusika, nyimbo zitakazopigwa kwa kufuata mpangilio(hapa utatakiwa kuongea na dj mapema), nyimbo zitakazokubalika kwa wahusika(sio taarab kwenye sherehe za kikristo, au kupiga nyimbo za akina rose muhando kwenye sherehe za waislam.

> Kuepuka kutamka maneno yanayoweza kuwafanya watu wajisikie vibaya, zungumza maneno yenye kufurahisha na kuchekesha.

> Vaa mavazi mazuri kulingana na tukio husika, mavazi ya staha ni muhimu.

> Kujiamini/jione Kuwa wewe unaweza na si kushindwa.

> Zingatia kwenda na muda, hapa utapatiwa script ya tukio zima na watu wa kamati ya harusi au hata birthday kisha na wewe unaweza kuandaa mwongozo wako kutegemea mwongozo (main script) utakayopewa, kama hakuna mwongozo basi unaweza kuutayarisha mwenyewe kwa kuwashirikisha wasimamizi wa tukio husika.

> Kuwashirikisha wageni waalikwa ili kuvuta usikivu wao na kuwafanya wajione nao ni wahusika muhimu; hapa utatakiwa kuandaa maswali ya kuwauliza wageni waalikwa kama vile......."..jamani bwana harusi amependeza au hajapendeza"? Ukishauliza utakaa kimya ili kusikia muitikio wao wa swali ulilowauliza.

> Ucheshi/uchangamfu.

ZINGATIA MUDA NA RATIBA.

asane sana jamani nashukuru
 
Back
Top Bottom