Mimba kutungwa nje ya mfuko wa uzazi hutokea pale yai lililorutubishwa kushindwa kujishikiza katika mji wa mimba(uterus) na kujishikiza katika mirija ya uzazi au sehemu nyingine ya tumbo.
Sababu zipo nyingi hizi ni baadhi kama magonjwa ya zinaa, maambukizi katika via vya uzazi (PID), uwepo wa kovu kama alishawai kufanyiwa upasuaji, matumizi ya dawa za uzazi n.k
Mwanamke anapokua na tatizo hilo hupata maumivu makali ya tumbo, kizunguzungu, kutapika na hutokwa na damu nyingi ukeni.
Mimba ikitungwa nje ya mji wake mtoto hawezi kusurvive mara nyingi mwanamke akikutwa na tatizo hilo hutibiwa kwa kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji.