Msaada, ni umri gani unafaa kumfundisha mtoto kareti?

mbere

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
6,967
Reaction score
6,465
Nimepanga uzao wangu wote lazima upitie huu mchezo, huyu mdogo ana miaka 3 kasoro, nimepanga kumpeleka pahala ajifunze
Umri unaofaa ni upi?
Unanishauri nini zaidi?
 
Any age,ila 3 is too young.Labda kuanzia 7-8 hivi, ideally 10
All in all ukimpeleka atleast aonyeshe interest nayo sio unamlazimisha
 
wapi wanafundisha watoto kareti?ningependa kufahamu
 
Nawashukuru sana
 
Nimepanga uzao wangu wote lazima upitie huu mchezo, huyu mdogo ana miaka 3 kasoro, nimepanga kumpeleka pahala ajifunze
Umri unaofaa ni upi?
Unanishauri nini zaidi?

Lengo lako haswa kama mzazi ni nini kwa huyo mwanao?
 
Kareti sio nzuri sana.. kuna kitu kinaitwa "Krav Maga" ndo wanayotumia askari, wanajeshi na wana intelligensia wa ki Israel. Ni mafunzo hatari sana hayo... sema sasa kwa hapa bongo sijui kama kuna walimu maana ni mafunzo ya Kiisrael
 
Nimepanga uzao wangu wote lazima upitie huu mchezo, huyu mdogo ana miaka 3 kasoro, nimepanga kumpeleka pahala ajifunze
Umri unaofaa ni upi?
Unanishauri nini zaidi?

Umri unaofaa ni kama huu alionao sasa Rais Mugabe.
Nakushauri tu anza kumzoesha Mwanao apende sana kuandamana na CHADEMA katika Mikutano yao na akiwa anapigwa pigwa sana " virungu " itampa picha halisi ni aina gani ya Karate za Kujifunza kwani na zenyewe pia zimegawanyika katika makundi mbalimbali.
Kila la kheri Mkuu na huyo Mwanao.
 
Kwanini miaka 7?
Hii ni kutokana na uzoefu wangu(binafsi nilianza na miaka 10).

Watoto wengi chini ya miaka 7 mazoezini walikua si wasikivu,wengine walikua wanalala kabla hata ya kuanza mazoezi.

Pia miaka mitatu viungo bado viteke mno,hivyo risk ya kuumia inakuwa juu hata kwa mazoezi unayofikiri ni madogo.
 
pia inategemeana na aina ya karate ila miaka mitano ni mizuri zaid kwa mtoto nasema hvyo coz nilianza hvyoo. ukipata dojo wanayofundisha KURENAI-KARATE au SHORINJ ni nzuri saana. Au mtaftie AIKIDO hyo ndo baba lao akicheza mwaka mmoja tuu vizuri na kipata wajapani wazuri aisee hata mkija 20 lazima ndani ya dk 10 muwe chali woote

but all in all kungfu is the best martial art, ungekuwa Dodoma kuna wachina wanafundisha SHAOLIN wapo njema saana na mitihani mnafanyia Hong Kong.
 
Kama kuna Dojo maeneo karibu na Temeke Dar tuambizane nimpeleke dogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…