Msaada, Nichukue kampuni ipi kati ya haya makampuni mawili ya mitambo ya umeme wa jua?

Tajiri Sinabay

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
1,333
Reaction score
3,619
Nahitaji kuchukua mtambo wa umeme wa jua wa kulipia kidogo kidogo.
nahitaji mtambo wa taa tano (bila TV)
Makampuni ambayo ni machaguo yangu ya mwanzo ni Sunking na Dlight.

Niliyogundua wakati nafanya tafiti ili kuona nichukue upi kati ya hii.

1. Sunking, uwezo wa mtambo wake wa taa ni mdogo ukilinganisha na mtambo wa taa tano wa Dlight.

2. Dlight, mtambo wake wa taa tano una uwezo mkubwa ukilinganisha na wa Sunking, changamoto sijajua uimara wa mitambo ya hawa Dlight.

Mwenye utaalamu ama uzoefu wa mitambo ya haya makampuni mawili na mengineyo yanayojihusisha na umeme wa jua naomba anisaidie tafadhali.
 
Tafuta inayoitwa Zola hutakuja kulalamika
 
Shukrani mkuu kwa ushauri, ila hawa zola kwa ninavyojua mimi mitambo yao midogo (isiyo na TV) mingi ni ile ya matoleo ya zamani sasa ile nimeiona kadha inapatwa na changamoto ya kuharibika kabla ya muda wa malipo kuisha.
na ukiwapigia kwa changamoto za hii mitambo midogo hawaji kutatua.

Sijajuwa kama wana matoleo mapya ya hii mitambo midogo, ngoja nicheki kwenye kurasa zao.
 
Ngoja waje wajuzi akina Rayns
 
Nahitaji kuchukua mtambo wa umeme wa jua wa kulipia kidogo kidogo.
nahitaji mtambo wa taa tano (bila TV)
Makampuni ambayo ni machaguo yangu ya mwanzo ni Sunking na Dlight.

Niliyogundua wakati nafanya tafiti ili kuona nichukue upi kati ya hii.

1. Sunking, uwezo wa mtambo wake wa taa ni mdogo ukilinganisha na mtambo wa taa tano wa Dlight.

2. Dlight, mtambo wake wa taa tano una uwezo mkubwa ukilinganisha na wa Sunking, changamoto sijajua uimara wa mitambo ya hawa Dlight.

Mwenye utaalamu ama uzoefu wa mitambo ya haya makampuni mawili na mengineyo yanayojihusisha na umeme wa jua naomba anisaidie tafadhali.
Hichi ulichokiandika kibiashara ni kitu cha kijinga na kipuuzi kabisa hapa JF. Jaribu kuwa real, acha kuwa fake. Hakukuwa na sababu yoyote ya kuja kuipigia debe kampuni ya Dlight kwa gharama ya kuchafua taswira ya kampuni zingine kama Sunking, Zola nk

Mleta mada acha utoto.
 
Bila kukuvunjia heshima mkuu, naheshimu sana michango yako humu jamii forums hasa kwenye jukwaa Technology ambako huwa nakuona sana.

Ila lirejee bandiko langu halafu ulinganishe na ulicho kiandika.

Kwanza nikwambie tu mimi nipo huku kusini. Ambako bila shaka kampuni ya Zola ndiyo kampuni inayoongoza kwa Mauzo kati ya makampuni yote ya umeme wa jua hapa nchini, naijua kwa mambo kadhaa kwenye ubora wake na mapungufu yake pia.

Pia kwenye post yangu ya kwanza hakuna mahali nimeitaja Zola, ila nimekuja kuizungumzia baada ya mdau hapo juu kunishauri kuhusu Zola.
Nahata nilipoizungumzia sikujitwisha ukamilifu kuihusu ndiyo maana nikasema ngoja nikaangalie kwenye kurasa zao ( nikimaanisha juu ya hii mitambo midogo)

Pia nimelinganisha mtambo wa taa tano wa kampuni ya Dlight una uwezo mkubwa ukilinganisha na Mtambo wa Sunking nikimaanisha Ukubwa wa battery zake, ila hata kwenye bei kuna utofauti.
Huo mtambo wa Dlight wa taa tano uko bei juu pia ukilinganisha na mtambo wa taa tano wa Sunking.

Nimejielezea sana hapo lakini lengo langu kubwa ni moja tu, ufute fikira ya kudhani naipigia bango kampuni yoyote.
 
Mimi mkuu labda nikupe wazo zaidi kama utapenda, Kwa Betri ya N9-10 inaweza kuwasha taa 2 na redio hizi bufa ndogo za 15W bila shida kabisa, jumlisha na solar yake ni around 50K hivi, so ukitenga Laki labda n ushee hivi, utawasha hizo taa 4 na simu utachaji bila bughudha ya malipo kila mwezi.

NB: Kupanga ni kuchagua, na uzuri wa solar unaweza anza pole pole.
 
Poa Poa kiongozi asante kwa ushauri wako
 
Mimi mkuu labda nikupe wazo zaidi kama utapenda, Kwa Betri ya N9-10 inaweza kuwasha taa 2 na redio hizi bufa ndogo za 15W bila shida kabisa, jumlisha na solar yake ni around 50K hivi, so ukitenga Laki labda n ushee hivi, utawasha hizo taa 4 na simu utachaji bila bughudha ya malipo kila mwezi.

NB: Kupanga ni kuchagua, na uzuri wa solar unaweza anza pole pole.
Safi kabisaa.
 
Bila kukuvunjia heshima mkuu, naheshimu sana michango yako humu jamii forums hasa kwenye jukwaa Technology ambako huwa nakuona sana.

Ila lirejee bandiko langu halafu ulinganishe na ulicho kiandika.

Kwanza nikwambie tu mimi nipo huku kusini. Ambako bila shaka kampuni ya Zola ndiyo kampuni inayoongoza kwa Mauzo kati ya makampuni yote ya umeme wa jua hapa nchini, naijua kwa mambo kadhaa kwenye ubora wake na mapungufu yake pia.

Pia kwenye post yangu ya kwanza hakuna mahali nimeitaja Zola, ila nimekuja kuizungumzia baada ya mdau hapo juu kunishauri kuhusu Zola.
Nahata nilipoizungumzia sikujitwisha ukamilifu kuihusu ndiyo maana nikasema ngoja nikaangalie kwenye kurasa zao ( nikimaanisha juu ya hii mitambo midogo)

Pia nimelinganisha mtambo wa taa tano wa kampuni ya Dlight una uwezo mkubwa ukilinganisha na Mtambo wa Sunking nikimaanisha Ukubwa wa battery zake, ila hata kwenye bei kuna utofauti.
Huo mtambo wa Dlight wa taa tano uko bei juu pia ukilinganisha na mtambo wa taa tano wa Sunking.

Nimejielezea sana hapo lakini lengo langu kubwa ni moja tu, ufute fikira ya kudhani naipigia bango kampuni yoyote.
Mkuu,sijajua Zola Kwa Sasa wamekuwaje ila mimi niliwachukulia wazazi wangu mtambo wa Zola tangu 2016 ila Hadi Sasa inadunda.
 
Back
Top Bottom