Nakushauri. Nimefuga kuku kwa zaidi ya miaka 10. Gharama kubwa ziko kwenye chakula. Na bei huwa zinapanda sana na hazieleweki.
Cha kwanza pata eneo la kutosha. Ifahamike kuwa sheria itakuja kuwabana wafugaji wa mijini kuhusu eneo la kufugia tafuta kuanzia hekari 5. Pia utaweza kupunguza gharama za chakula kwa kuotesha baadhi ya vitu vinavyohitajika ikiwa ni pamoja ma majani kama mlonge au lukina au mulberry. Pia kama ni wa kienyeji utaweza kuwatoa nje wajitaftie.
Cha pili jenga banda ambalo litapunguza magonjwa na hivyo kukupunguzia matumizi ya madawa. Cha tatu ili mradi wa kuku ukupe faida nono uunganishe na miradi mingine mfano mradi wa bustani na uzalishaji wa biogas au miradi mingine inayohusiana.
Hapa nitaweka kiambatanisho cha kuonyesha mfumo wenyewe ukoje. Chakula kinachukua asilimia kubwa sana hivyo ni vyema mfugaji akawa na stock ya kutumika muda mrefu au akaagiza moja kwa moja kutoka kiwandani ikiwa anafuga kwa kiwango kikubwa