Msaada: Nifanyaje ili biashara ya kuku inipe mafanikio ya kimaisha

Msaada: Nifanyaje ili biashara ya kuku inipe mafanikio ya kimaisha

Nakushauri. Nimefuga kuku kwa zaidi ya miaka 10. Gharama kubwa ziko kwenye chakula. Na bei huwa zinapanda sana na hazieleweki.

Cha kwanza pata eneo la kutosha. Ifahamike kuwa sheria itakuja kuwabana wafugaji wa mijini kuhusu eneo la kufugia tafuta kuanzia hekari 5. Pia utaweza kupunguza gharama za chakula kwa kuotesha baadhi ya vitu vinavyohitajika ikiwa ni pamoja ma majani kama mlonge au lukina au mulberry. Pia kama ni wa kienyeji utaweza kuwatoa nje wajitaftie.

Cha pili jenga banda ambalo litapunguza magonjwa na hivyo kukupunguzia matumizi ya madawa. Cha tatu ili mradi wa kuku ukupe faida nono uunganishe na miradi mingine mfano mradi wa bustani na uzalishaji wa biogas au miradi mingine inayohusiana.

Hapa nitaweka kiambatanisho cha kuonyesha mfumo wenyewe ukoje. Chakula kinachukua asilimia kubwa sana hivyo ni vyema mfugaji akawa na stock ya kutumika muda mrefu au akaagiza moja kwa moja kutoka kiwandani ikiwa anafuga kwa kiwango kikubwa

Mkuu nimekupata vizur sana ilaa nataka ni focus hasa kwenye soko la mayai, hasa kuliko kumuuza kuku mwenyewe.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Write your reply. Hongera kwa kuweza kuaanza kufuga. Ushauri wangu ninkuwa ungeanza na kuku wa lika moija (the same age) ua hapo wangeanza kutaga wakauyu mmoja na hapo ugeweza kupata tray 1.5 kila siiku. kama unaweza kuanza upya anza na kuku 100

Ili niweze kupata atleast tray 1 kwa siku itabid niwe na matetea wangapi?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Fuga broilers, uwe unauza baada ya mwezi..
Kuroilers wanakula Sana sana, Nina experience nao Sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa mkuu, unaweza kunisaidia jinsi gani naweza kupunguza gharama ya chakula?

Naona, kweli kwenye swala la msosi it's very expensive sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
pata elimu sahihi ya ufugaji itakuongoza kufikia ndoto

Ndio maana nimekuja humu, nipate elimu na maarifa kutoka kwa wataalam.. Naamin wataalam humu wapo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama chakula unatengeneza mwenyewe nunua vichanganyio vyako kwenye duka la jumla.
Kama unanua kilichotoka kiwandani chagua aina nzuri sana. Walishe kwa kipimo kutokana na umri wao kutokana na umri kila kuku anakula chakula cha uzito fulani kwa siku. Pia hakikisha hawamwagi kabisa chakula.yaani wale chakula chote.
Vyombo vya chakula vya dukani haviwezi kukusaidia hilo. Itabidi utengeneze hivyo vyombo mwenyewe. Wape dawa ya minyoo kwa wakati kuzuia minyoo maana hupunguza utagaji. Wakague kuhakikisha hawana wadudu kwa nje , chawa, viroboto etc. Wawekee vutagio vya kutosha. Hakikisha wana maji ya kunywa muda wote. Watundikie majani mabichi au wawekee vitamini kwenye maji walau mara tatu kwa wiki
Sasa mkuu, unaweza kunisaidia jinsi gani naweza kupunguza gharama ya chakula?

Naona, kweli kwenye swala la msosi it's very expensive sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ili niweze kupata atleast tray 1 kwa siku itabid niwe na matetea wangapi?


Sent from my iPhone using JamiiForums
Ili niweze kupata atleast tray 1 kwa siku itabid niwe na matetea wangapi?


Sent from my iPhone using JamiiForums

at least itakubindi uwe na mitetea 40 na wanapata chakula bora na maji safi pia hawasumbuliwi na magonjwa
 
Back
Top Bottom