msaada nikinywa beer 2 tumbo linakuwa limejaa

msaada nikinywa beer 2 tumbo linakuwa limejaa

kwel2

Senior Member
Joined
Dec 30, 2012
Posts
109
Reaction score
47
jaman watalamu miye ni mnyaji mzuri wa beer kuanzia nane mpaka kumi na zaidi ila kwa sasa nikinywa beer 2 tu nahisi tumbo kujaa inamaana beer ya tau siwezi kuinya sijajua tatizo ni nini
 
Kunywa Kisu a.k.a Radi a.k.a Kachasu almaarufu Konyagi Mwitu no 1 itakusaidia kukurudisha Barabarani. Hilo tatizo sometimes linasababishwa na bia ambazo hazjaiva. Alaf kama ulikua unakunywa moto badili na anza tumia za Bridiiiiiiiii.
 
Mungu ana njia nyingi za kukuonyesha ubaya wa kitu Mkuu.. Huitaji mtaalam kukuambia sababu achana na vilevi maana hakika Yeye ameona madhara ya baadae kwako..
 
Utakuwa una gesi tumboni ambayo itapelekea vidonda vya tumbo.

Jaribu kutumia Kabichi na matango kwa wingi utaondokana nayo. Japo inaonaekana ukomo wako wa kunywa bia umekaribia na sie wenzio tulianza hivyo hivyo, mara tumbo limejaa, kichwa kinauma, mara unaharisha, wife anakupigia kelele unanuka pombe, watoto wakikuona wanasema "dadiee you like most drinking than us.." kanisani ukianeda unasinzia, jamaa wanacheka hukulala home, ofisini jamaa wanakuona kama haupo responsible ...baadae unajikuta pombe haina tija..unaachana nayo...
 
Tatizo dogo sana hilo, changanya na viroba mambo yatakuwa sawa
 
Mungu ana njia nyingi za kukuonyesha ubaya wa kitu Mkuu.. Huitaji mtaalam kukuambia sababu achana na vilevi maana hakika Yeye ameona madhara ya baadae kwako..
Hivi kunywa pombe ni dhambi? If yes toa supportive facts mkuu to prove ua assertion......
 
Acha kunywa bia uone kama tumbo litajaa tena.

Jamaa hajataka kuacha ndio maana anaulizia remedy ya tatizo wakati bado anapata Lager yake!

Usimfanye mwenzetu atuache peke yetu huko Kaunta Zion Daughter jamani!
 
Hivi kunywa pombe ni dhambi? If yes toa supportive facts mkuu to prove ua assertion......

Mkuu Vmark kuna sehemu ambayo mie nimesema pombe ni dhambi..? Lakini pombe hiyo hiyo ci ndo inajulikana kwa kuwa chanzo cha mabaya mengi..? Kutukana.. kushawishi kutenda dhambi za uasherati.. zinaa.. Zinachochea kuvunja familia.. Kupoteza kipato.. kuwa mzembe kazini.. kukutia ujinga na mengine mengi..! Na upo ushahidi wa kitafiti unaonyesha pombe na haswa pombe kali zinachangia kuliharibu ini..
 
Kunywa bia moja, hela inayobakia kwenye wallet kanunue tofali uweke mahali. Otherwise kwa tiba ya kudumu tafuta nyumba uingie mortgage tu yaishe.
Pole na kila la kheri.
 
Hivi kunywa pombe ni dhambi? If yes toa supportive facts mkuu to prove ua assertion......
Kweli kabisa, jamaa hapa kaomba msaada kiafya sasa wenzetu wengine wanajoki tu hapa, hii si sawa. Tumsaidie kama mtu huna utaalamu ni bora UPITE tu.
 
Mkuu Vmark kuna sehemu ambayo mie nimesema pombe ni dhambi..? Lakini pombe hiyo hiyo ci ndo inajulikana kwa kuwa chanzo cha mabaya mengi..? Kutukana.. kushawishi kutenda dhambi za uasherati.. zinaa.. Zinachochea kuvunja familia.. Kupoteza kipato.. kuwa mzembe kazini.. kukutia ujinga na mengine mengi..! Na upo ushahidi wa kitafiti unaonyesha pombe na haswa pombe kali zinachangia kuliharibu ini..
Huwa mtu kadhamiria kabla kwa hiyo anataka huruma kwa kusingizia pombe. Je uliisha sikia JAMBAZI likiilaumu pombe kuwa ndio iliyomtuma?
 
Huwa mtu kadhamiria kabla kwa hiyo anataka huruma kwa kusingizia pombe. Je uliisha sikia JAMBAZI likiilaumu pombe kuwa ndio iliyomtuma?

Wapo wanaodhamiria hivyo lakini wapo wengi ambao once wakishakunywa pombe baci akili zinakuwa sio zao tena.. Wanafanya mengi ambayo baadae wakija kuwa sober hawaamini kama walifanya vituko vya ajabu.. Well kwa jambazi kulaumu pombe mbona wengi tu.. Sema kwa style tofauti.. Wengi wanafanya ujambazi wakaweke heshima bar..
 
Back
Top Bottom