Msaada: Niko njia panda, niendelee na mishe zangu au niombe ajira za Serikali?

Msaada: Niko njia panda, niendelee na mishe zangu au niombe ajira za Serikali?

Son.j

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2013
Posts
1,010
Reaction score
2,356
Husika na mada hapo juu. Mimi ni mhitimu wa diploma ya elimu since 2017. Mwaka 2019 nikaaply degree na nilichaguliwa lkn sikwenda baada ya kuwaza sana nikaona nifanye mishe kwanza kwa hela kidogo nliyonayo badala ya kupoteza 3 yrs chuo alaf nianze kuhangaika na ajira, nikiwaza kwamba nitaenda kusoma nikishaajiriwa nikiwa kazini yaan.

Nikaanza biashara mambo hayakuwa mazuri sana lkn kadri sku znavoenda mambo yakaanza kunyooka, miaka yote hiyo nilikuwa na apply pale nafasi zinapotangazwa, hata hivo nilikuwa nafanya biashara kwa mtazamo kwamba ipo siku ntaondoka tu kwahyo skuwa committed saaaana(thing that i regret) coz mwaka jana nlipokosa ajira nkajitosa nkaweka nguvu kubwa kwenye kazi nnayofanya ikiwemo kuboresha ofice na kununua mashine za kazi, ambapo sasa hivi naona return ya effort nliyoweka last year, since nna uhakika wa kupata profit ya 20-30k per day. Nkaanza kutoa wazo la ajira kichwani until now.

The thing here is.
*Kwenye biashara soko linayumba sana nowdays(nafanya biashara ya vifaa vya simu)
*kwenye biashara kuna ushindani hadi kulogana kupo
*kuna matukio ya uwizi na moto kitu ambacho in a single morning unafungua milango unajikuta maskini huna kitu kabisa.. gone
*kodi nazo zinapanda hasa za TRA pia kunakutolewa kwenye pango ulilopo, location ina matter. Yaani hapo sina uhakika.

Kwenye ajira.
*Since ni ualimu probably ntapangiwa kijijini sana ambapo fursa ni chache na changamoto ni nyingi.
*kuutegemea tu mshahara as income yani mwezi to mwezi
*kazi ni ngumu( imagine kumtoa mtu ujinga) na utakuta darasa lina wanafunzi 269 huko
After all japo ualimu ni wito but Tumbo first jamani.

Mambo ni mengi wapendwa ila mimi kwa ufupi nimeshayapenda haya maisha nnayoyaishi sasa, am just curious about a future. Mnishauri wenzenu nikomae au ni apply tu

N.B sijawaza kufanya vyote since biashara kwa sasa usipo simamia mwenyewe unakula hasara nzuri tu.
 
Mkuu , kama unataka utajiri, komaa na biashara, ila kama unataka maisha ya kawaida tu, basi apply kazi serikalini.. Fanya hivi, kama sasa hivi unapata 30k per, basi ongeza bidii na ubunifu kwenye biashara yako, kipato kiwe kinaongeza, kuanzia 30 mpka 50k per, make sure graph yako inapanda..

Hapo, unaweza ukafungua duka la pili, then mambo yatakuwa yana ji sort , na uta enjoy game la kujiajiri, tumia changamoto kama chachu, ya kujifunza na kupata experience kwenye sekta ya ujasiriamali..
 
Assume tu kuwa ukiapply utakosa, then komaa na biashara au kama unahis ukimuajiri mtu hapo atamanage vizuri basi apply. Afu kwann unajipa uhakika kuwa utapata this time.
 
Shukran sana kwa mawazo yko
 
Assume tu kuwa ukiapply utakosa, then komaa na biashara au kama unahis ukimuajiri mtu hapo atamanage vizuri basi apply. Afu kwann unajipa uhakika kuwa utapata this time.
Kuajiri mtu hapana hilo nimeshalifuta kabisa labda km nitakuwepo hapa hapa, and siamini kuwa nitapata ila nikiapply kuna mawili lkn nisipoapply ni kwamba nimechagua moja.
 
Komaa hapo hapo unapopata ridhiki huku ukijitahidi kuboresha kadiri unavyopata uzoefu. Usirudi nyuma kufikiria mambo ya ajira
 
Komaa tu na mishe yako. Hizo changamoto ni chakula cha ubongo wa mpambanaji kama wewe.
 
Uzuri wanaokushauri wote Wameajiriwa so wanatoa ushuhuda ambao reality hawaijui

Ukitaka kujua ugumu wa ndoa uliza mwanamke aliyeachika usiulize aliye kwenye ndoa
 
Bora ukaendelea kupambana mtaani. Tayari umeshajaribu na umeona mwanga. Jiajiri uwe Bosi, au nenda kaajiriwe ili uwe mtumwa maisha yako yote.

Changamoto kwenye biashara ni jambo la kawaida.
Ujumbe murua
 
Changamoto na ugumu kwenye chochote kile ni kitu cha kawaida na hauwezi kuzikimbia, na probably unapokwenda utakutana na changamoto zenye ugumu uleule.
Ni bora uwe na focus, commitment na kitu kimoja kwa nguvu zote na upate jibu moja, kuliko ufanye vingi ambapo ni lazima utakosa vyote.

Maisha yanahitaji consistency.
 
Uzuri wanaokushauri wote Wameajiriwa so wanatoa ushuhuda ambao reality hawaijui

Ukitaka kujua ugumu wa ndoa uliza mwanamke aliyeachika usiulize aliye kwenye ndoa
😄😄😄
 
Changamoto na ugumu kwenye chochote kile ni kitu cha kawaida na hauwezi kuzikimbia, na probably unapokwenda utakutana na changamoto zenye ugumu uleule.
Ni bora uwe na focus, commitment na kitu kimoja kwa nguvu zote na upate jibu moja, kuliko ufanye vingi ambapo ni lazima utakosa vyote.

Maisha yanahitaji consistency.
Nimeipat point yako nashkuru sana
 
kuajiriwa, ni kuchagua kutumia muda mwingi kutumikia watu/kampuni/taasisi/idara.
kujiajiri, ni kuchagua kutumia muda mwingi kutimiza mipango yako mwenyewe huku ukikubali kukabiliana na changamoto.

chagua, ila angalia usije kujilaumu mwenyewe.
 
Ukitaka uzeeke mapema na kizazi chako kiwe maskini kuwa mtumishi wa serikali hasa chini ya Tamisemi
 
Back
Top Bottom