Msaada: Nimeagiza pick up chasis imekatika kwa kutu

Entim

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
4,025
Reaction score
2,261
Wakubwa shikamooni,

Mimi ni mjasiriamali, naombeni msaada kwa wale wataalamu wa magari.
Leo hii nimetoka kulipia bandarini (TPA) used 1996 hillux double cabin (petrol engine 2000cc) nimenda service nimegundua chasis imeliwa na kutu about 35% kwa upande wa mbele.

Nimejaribu kuomba ushauri nazidi kuchanganyikiwa maana gari yenyewe imenicost tsh 33m (cif+import tax na fine ya uchakavu 3.5m) Fundi wa kwanza ananishauri nikate nusu nikanunue spare nichomelee, wa pili kasema niungeunge hivyohivyo, wa tatu kashauri nishushe chasis nzima niweke mpya.

Naombeni maoni yenu, kejeli na vijembe vitauwa bure pressure imepanda haswa.

Nawasilisha.
 
Mod please nisaidie kupandisha huu uzi na ubaki pale juu hadi weekend..[emoji26]
 
Hukulipia ukaguz ikiwa kulekule, nashauri weka mpya
 
Mod please nisaidie kupandisha huu uzi na ubaki pale juu hadi weekend..[emoji26]
Zingatia ushauri watatu.
Sio salama kuunga chassis, weka chassis nzima
 
Bei gani mkuu? Thanks
pale shauri moyo Dar es saaam wanakatakata magari mengi nenda uta negotiate ni vyema ukazunguka maduka mengi tofauti tofauti kwa siku tofauti tofauti utapata tu ya bei zuri yenye kiwango pia.
 
Thanks, nzima inaweza kuwa bei gani mkuu?
Inategemea na hali yake, jaribu uhuru road ukitokea round about baada ya benjamini mkapa...duka limeandikwa KOYO huyu jamaa ana magari ya kila aina yaliyochinjwa atakusaidia..ni maarufu sana..laki 3 hadi 5
 
Nashukuru sana,
 
Entim

Nafikiri sasa ifike wakati waagiza magari ndani ya nchi wajue haki zao.

Nilishawahi kuagiza gari ikawa Ina matatizo. Kampuni iliyoniuzia ni Be forward.

Nikaja kufahamu ukinunua gari kupitia wakala wao huwa wanamshauri achague gari lingine iwapo gari alilochagua ni bovu ila kama ni mara ya kwanza kuagiza na hukuomba kujua hilo gari lina tatizo gani basi wanakubambika.

Unaweza kabisa kuishtaki kampuni iliyokuuzia gari bovu na kama hawakusema hilo gari lina tatizo mwanzoni. Kwenye mashtaka unawaingiza pia wale wakaguzi.

Miaka ya nyuma sana mzee wangu alikuwa na canter. Chassis ikawa imeliwa na kutu. Alichofanya aliunga zile sehemu zilizooza, lakini pia alinunua Mbao za mninga original akazungushia juu ya chassis halafu akazifunga na u-bolt. Hapo hata spare used zilikuwa hazipo.

Nashauri uende shauri moyo pale ilala ukaulizie bei. Pia unaweza kutembelea garage maarufu kama za wachina kuomba ushauri.
 
Mkuu, huu jamaa inaelekea hajaenda kwa wakala kabla hajalipa, mim nilienda kw wakala akanizui kulipia gari nilillochagua kumbe lilikuwa ina vuja oil, nikachagua lingine

Ndiyo hivyo mkuu. Ni kutokujua. Ila mteja ana haki ya kujulishwa ubovu wa gari kabla ya kununua na hata kupewa log book ya matengenezo.

Kwa wenzetu ni kesi kubwa na kuna Sheria zake kabisa.
 
Mkuu pole sana!mambo ya kuagiza magari online ni changamoto,hebu tuwekee hapa mtandao ulioagizia mkuu ili wadau waujue manake hii ni kesi yetu sote mkuu,mimi nliagiza gari kwenye tradecarview nlikua sina amani hata kidogo,ila gari ilipoingia ilikua ni ile ile nliyoiona!
 
Entim

Nafikiri sasa ifike wakati waagiza magari ndani ya nchi wajue haki zao.

Nilishawahi kuagiza gari ikawa Ina matatizo. Kampuni iliyoniuzia ni Be forward.

Nikaja kufahamu ukinunua gari kupitia wakala wao huwa wanamshauri achague gari lingine iwapo gari alilochagua ni bovu ila kama ni mara ya kwanza kuagiza na hukuomba kujua hilo gari lina tatizo gani basi wanakubambika.

Unaweza kabisa kuishtaki kampuni iliyokuuzia gari bovu na kama hawakusema hilo gari lina tatizo mwanzoni. Kwenye mashtaka unawaingiza pia wale wakaguzi.

Miaka ya nyuma sana mzee wangu alikuwa na canter. Chassis ikawa imeliwa na kutu. Alichofanya aliunga zile sehemu zilizooza, lakini pia alinunua Mbao za mninga original akazungushia juu ya chassis halafu akazifunga na u-bolt. Hapo hata spare used zilikuwa hazipo.

Nashauri uende shauri moyo pale ilala ukaulizie bei. Pia unaweza kutembelea garage maarufu kama za wachina kuomba ushauri.
Nashukuru sana. Nina inspection certificate na kwa sasa nangalia possibility ya kuwapeleka mahakamani. Ila response yao ya leo eti wanadai kuwa used car has no gurantee. Hivyo kwa kupitia jukwaa hili naweza kusema mimi nimekuwa victim l, na wanaoagiza magari watumie muda mwingi kukagua na kuwauliza wauzaji kuhusu chasis.
 
Mkuu pole sana!mambo ya kuagiza magari online ni changamoto,hebu tuwekee hapa mtandao ulioagizia mkuu ili wadau waujue manake hii ni kesi yetu sote mkuu,mimi nliagiza gari kwenye tradecarview nlikua sina amani hata kidogo,ila gari ilipoingia ilikua ni ile ile nliyoiona!
Tradecarview ni mnada hivyo inakuwa na mkusabyiko wa makampuni mengi. Link nitaupload
 
pale shauri moyo Dar es saaam wanakatakata magari mengi nenda uta negotiate ni vyema ukazunguka maduka mengi tofauti tofauti kwa siku tofauti tofauti utapata tu ya bei zuri yenye kiwango pia.
Lol asante sana. Maana nikifika Iringa sidhani kama nitapata hii huduma za chasis
 
Nashukuru sana. Nina inspection certificate na kwa sasa nangalia possibility ya kuwapeleka mahakamani. Ila response yao ya leo eti wanadai kuwa used car has no gurantee. Hivyo kwa kupitia jukwaa hili naweza kusema mimi nimekuwa victim l, na wanaoagiza magari watumie muda mwingi kukagua na kuwauliza wauzaji kuhusu chasis.
Kinachotusababishia watanzania wengi tuache kwenda mahakamani nafikiri ni usumbufu.

Hata kama gari ni used na haina guarantee lakini walitakiwa kukupa facts za hali ya gari na hata picha za sehemu mbovu ili ufanye uamuzi sahihi.

Lakini kama ulinunua kwenye mnada issue inakuwa ngumu kwani lazima lawyer aanzie huko kama hao wauzaji hawana ofisi hapa bongo.

Pole mkuu.
 
Back
Top Bottom