Msaada: Nimeagiza pick up chasis imekatika kwa kutu

Msaada: Nimeagiza pick up chasis imekatika kwa kutu

fata ushauri wa fundi wa tatu. na katika mafundi wako huyo ndiyo bora zaidi sababu hataki kukupa hasara mara mbili
 
Mkuu pole sana!mambo ya kuagiza magari online ni changamoto,hebu tuwekee hapa mtandao ulioagizia mkuu ili wadau waujue manake hii ni kesi yetu sote mkuu,mimi nliagiza gari kwenye tradecarview nlikua sina amani hata kidogo,ila gari ilipoingia ilikua ni ile ile nliyoiona!
Trade car view gari zao hua expensive kidogo kulinganisha na be forward lkn uzuri wake zinakua Na km chache
 
Nashukuru sana. Nina inspection certificate na kwa sasa nangalia possibility ya kuwapeleka mahakamani. Ila response yao ya leo eti wanadai kuwa used car has no gurantee. Hivyo kwa kupitia jukwaa hili naweza kusema mimi nimekuwa victim l, na wanaoagiza magari watumie muda mwingi kukagua na kuwauliza wauzaji kuhusu chasis.
Pole Mkuu, hata kama ni used walitakiwa kukuambia ukweli ili ukubaliane nao, mitandao/makampuni mengine huwa yanaonyesha kwa picha hata sehemu zenye scratch ili ukubaliane nayo, ni kwa nini wao hawakukuonyesha hilo, ina maana walikuwa na nia ovu. Wasiliana na wanasheria, watakushauri cha kufanya, kama vipi nenda kalalamike Ubalozini kwao. Siku nyingine tumia wale Wakala wa malipo yaani Paytrade
 
mkuu pole sana nunua chassis ingine yote iunge na ipakwe rangi. ya kuzuia kutu kabla haijaungwa..Wajapani ni matapeli sana gari ya 1996 inagharimu 33milioni? South Africa unaweza kupata toyota hilux d4d ya 2005 mpaka 2007, 2008-2012 ukiwa na 40m inaingia Tanzania pamoja na kodi.. Wajapani Mungu anawaona gari ya 1996 wanauza bei hiyo pamoja na kodi au mimi sijaelewa..huko hawazingatii umri wa gari kushusha bei? duh pole sana
 
Next time nenda SBT, ila mkuu mil33 palefu, ungevizia mi hilux used ya serikali au ya wakimbizi ungepata kwa bei ndogo sana.
 
Wakubwa shikamooni,

Mimi ni mjasiriamali, naombeni msaada kwa wale wataalamu wa magari.
Leo hii nimetoka kulipia bandarini (TPA) used 1996 hillux double cabin (petrol engine 2000cc) nimenda service nimegundua chasis imeliwa na kutu about 35% kwa upande wa mbele.

Nimejaribu kuomba ushauri nazidi kuchanganyikiwa maana gari yenyewe imenicost tsh 33m (cif+import tax na fine ya uchakavu 3.5m) Fundi wa kwanza ananishauri nikate nusu nikanunue spare nichomelee, wa pili kasema niungeunge hivyohivyo, wa tatu kashauri nishushe chasis nzima niweke mpya.

Naombeni maoni yenu, kejeli na vijembe vitauwa bure pressure imepanda haswa.

Nawasilisha.
Hebu fatilia vizuri huo ushauri wa tatu uliopewa, nadhani Unapoweka chasis nyingine tayari hiyo gari inakuwa nyingine kiserikali, nadhani kwa sasa Kiserikali unaweza kubadirisha engine lakini sio chasis, fatilia kwanza mkuu usije ingia kwenye shida siku za mbele

Njia nzuri ni kuirepea hiyo chasisi wapo watu wenye uwezo huo wa kuifanya chasisi yako iwe kwenye hali nzuri tu
 
Hebu fatilia vizuri huo ushauri wa tatu uliopewa, nadhani Unapoweka chasis nyingine tayari hiyo gari inakuwa nyingine kiserikali, nadhani kwa sasa Kiserikali unaweza kubadirisha engine lakini sio chasis, fatilia kwanza mkuu usije ingia kwenye shida siku za mbele

Njia nzuri ni kuirepea hiyo chasisi wapo watu wenye uwezo huo wa kuifanya chasisi yako iwe kwenye hali nzuri tu
Uuuwi, kumbe? NDOO MAANA KWENYE KADI KUNA CHASIS # ENHEE??
 
Back
Top Bottom