Msaada: Nimeagiza pick up chasis imekatika kwa kutu

fata ushauri wa fundi wa tatu. na katika mafundi wako huyo ndiyo bora zaidi sababu hataki kukupa hasara mara mbili
 
Trade car view gari zao hua expensive kidogo kulinganisha na be forward lkn uzuri wake zinakua Na km chache
 
Pole Mkuu, hata kama ni used walitakiwa kukuambia ukweli ili ukubaliane nao, mitandao/makampuni mengine huwa yanaonyesha kwa picha hata sehemu zenye scratch ili ukubaliane nayo, ni kwa nini wao hawakukuonyesha hilo, ina maana walikuwa na nia ovu. Wasiliana na wanasheria, watakushauri cha kufanya, kama vipi nenda kalalamike Ubalozini kwao. Siku nyingine tumia wale Wakala wa malipo yaani Paytrade
 
mkuu pole sana nunua chassis ingine yote iunge na ipakwe rangi. ya kuzuia kutu kabla haijaungwa..Wajapani ni matapeli sana gari ya 1996 inagharimu 33milioni? South Africa unaweza kupata toyota hilux d4d ya 2005 mpaka 2007, 2008-2012 ukiwa na 40m inaingia Tanzania pamoja na kodi.. Wajapani Mungu anawaona gari ya 1996 wanauza bei hiyo pamoja na kodi au mimi sijaelewa..huko hawazingatii umri wa gari kushusha bei? duh pole sana
 
Next time nenda SBT, ila mkuu mil33 palefu, ungevizia mi hilux used ya serikali au ya wakimbizi ungepata kwa bei ndogo sana.
 
Hebu fatilia vizuri huo ushauri wa tatu uliopewa, nadhani Unapoweka chasis nyingine tayari hiyo gari inakuwa nyingine kiserikali, nadhani kwa sasa Kiserikali unaweza kubadirisha engine lakini sio chasis, fatilia kwanza mkuu usije ingia kwenye shida siku za mbele

Njia nzuri ni kuirepea hiyo chasisi wapo watu wenye uwezo huo wa kuifanya chasisi yako iwe kwenye hali nzuri tu
 
Uuuwi, kumbe? NDOO MAANA KWENYE KADI KUNA CHASIS # ENHEE??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…