Nafikiri niseme ni word ila siyo kwenye pc ni kwenye simu.
Document yako ina jina tuassume jina la document ni Uvuvi Kigogo.
Hii document ili iwe determined ni aina gani hua inaangaliwa extension so mfano ni PDF itakua na jina Uvuvi Kigogo.pdf.
Kama ni word itakua na jina Uvuvi Kigogo.doc
Kama ni excel itakua Uvuvi Kigogo.xlsx
Ndiyo maana nimeuliza extension yake ili tuanze kudeduce kwanini kwenye PC itokee viboksi.
Njia rahisi fanya kama unarename hiyo document mwishoni kabisa utaona extension yake.
Now fanya hivi;
Kwakua kwenye simu inaonekana.
Ingia online search hivi 'word to pdf'
Zitakuja sites mbalimbali zinazoweza kufanya hiyo kazi ambazo hazina mushkeli ni sodapdf, smallpdf yaani zile za mwanzoni.
Ingia katika site mojawapo. Utaelekezwa pa kuiweka doc yako. Convert hiyo doc kwenda kwenye pdf.
Idownload.
Iweke kwenye PC cheki kama inaonekana. Kama unaiona, basi copy hiyo doc nzima na ipaste kwenye word.
Hapa utakua na kazi ya kuhariri hapa na pale. Ni bora kuliko kubaki na viboksi.