Msaada: Nimefanya clearance lakini mwajiri akaninyima barua ya kuachishwa kazi

Msaada: Nimefanya clearance lakini mwajiri akaninyima barua ya kuachishwa kazi

abagabo

Senior Member
Joined
Jun 4, 2014
Posts
155
Reaction score
168
Nimeachishwa kazi na mwajiri na akanipa clearance form, nimefanya clearance na kukabidhi kila kitu, jambo ajabu kaninyima barua ya kuniondoa kazini. Anadai eti ataniita kwenye kamati ya ajira na nidhamu ili wanihukumu; swali

1. je nini maana ya kufanya clearance kisheria?
2. mwajiri kuniambia ataniita, je ataniita kama mwajiriwa au mtu wa mtaani?
3. Ni haki gani kisheria?

Suala ili sasa limefikisha miezi 9 tangu litokee na mimi ni mtu wa singida kimakazi na mwajiri yupo musoma.
msaada wa tafadhali
 
sasa limefikisha miezi 9 tangu litokee na mimi ni mtu wa singida kimakazi na mwajiri yupo musoma.
msaada wa tafadhali
Mwajiri yupo musoma! Naomba nikuulize, anakuachisha vipi kazi wakati huna barua ya kuachishwa kazi na kosa lipi ? Ni serikali au private?
 
Ukiacha kwenda kazini utakuja kufukuzwa kazi kwa utoro wewe.


Kama hujapewa barua ya kuachishwa kazi endelea kwenda kazini kama kawaida.
 
Unachokiongea kama ukweli na ukweli mtupu, basi you have a strong case against your 'employer' maana taratibu hazijafatwa, hata akiita disciplinary committee bado unaye kwasababu tiyari yeye ameishafikia maamuzi. Taarifa ulizotoa sio kamilifu hence can not be the basis of legal advice. Find the advise of an attorney for advice.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom