Hujaishiwa nguvu za kiume mkuu...
Kilichotokea ni kushuka kwa hormone ya kiume inaitwa testosterone.
Hormone hii inakuwa iko juu sana kijana anapoingia miaka kuanzia 18 mpaka 21, lakini wengne huchelewa mpaka wanapogonga 30.
Kwa kawaida inatakiwa hormone hii ishuke mara tu unapofika miaka 30 kwa kiwango cha 1% au 2% kwa mwaka, lakin wengine hushuka kwa haraka sana kwa sababu nyingi mno.
Lazima uangalie lifestyle yako kama inasababisha kushuka kwa hormone hii ikiwemo pombe au stress au sectual motivation au kula vyakula vyenye hormone ya kike kwa wingi inayoitwa estrogen.
Estrogen ni hormone ya kike inayoleta tabia za kike na Testosterone ni ya kiume inajenga mambo ya kiume, kawaida mazingira yana mpambano wa kila siku wa hormone ya kiume na kike, ambapo ya kiume ikizidi unakuwa na tabia nyingi a kiume na maumbile ya kiume kweli kweli, mambo kama kupiga show za kibabe, mambokama kumwaga bao jingi mpaka unajishangaa, mambo kama sauti nzito, mambo kama kuwa rough sana na kutojipenda, mambo kama kujenga misuli ya mwili mambo kama hasira za kupenda ugomvi na mengineyo.
Za kike zikizidi unaanza kujenga mambo ya kike kama kupenda utulivu wa kukaa nyumbani na kuangalia tamthilia za mapenzi asubuhi mpaka jioni, mambo kama kupenda ubuyu, mambo kama kuvimba kwa matiti na kuwa na chuchu za kike wakati wewe mwanaume , mambo kama kupungua kwa ashki za ngono, uume kupungua kusimama nyakati za asubuhi na vitu vingine.
Unatakiwa upambane upate balance ya hormone katika mwili, kwa maana ya kuhakikisha hauli vyakula vyenye kuleta sana hormone ya kike na kupendelea kula vyakula vyenye hormone ya kiume.
Punguza pombe, vyakula vya kukoboa, punguza stress, punguza sigara, punguza kunywa soda sana, punguza kuala masaa machache, punguza sukari kwenye vyakula vyako.
Lakini kumbuka pia kupungua kwa hormone hii ni jambo la kawaida kiafya, tatizo linapokuja ni pale inaposhuka kwa haraka.
Pia kumbuka mwili una hormone zote za kiume na kike.