Ivan Breaker
JF-Expert Member
- Jun 13, 2020
- 1,379
- 5,499
...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uza huo muda wa maongezi hakuna namna ya kupata hela yako zaidi ya kuuza vocha.Ilikuwa ni siku ya jana majira ya Jioni, nikiwa nyumbani niliona bidhaa mtandaoni na nikaipenda nikaamua kuwasiliana na waliokuwa wameitangaza katika mtandao wa Instagram. Nilifanikiwa kuwasiliana nao na nikaomba wanifanyie Delivery hadi nyumbani.
Sasa wakati boda wa Delivery amefika nyumbani, nikawa nataka kufanya malipo yake kwa sababu sikuwa na Cash na nilikuwa na pesa kwenye Bank nikaamua kuhamisha Pesa kutoka Bank kuja kwenye simu ili niweze kulipa kupitia LIPA NAMBA yao na hapo ndipo nilipokuja kukosea badala ya kutuma pesa nikanunua muda wa maongezi wa Tshs 100,000/= 🥴. Pale Pale biashara iliishia pale na nikaanza kutafta namna ya kurudisha pesa imeshindikana hadi sasa
Hivyo naomba msaada kwenu wataalamu nifanye nini? au kama kuna mtu ambaye anahusika nw kutoa huduma za kurusha vifurushi naomba tuwasiliane tufanye biashara nipo tayari ata niingie hasara ya kiasi fulani.
Au mwenye msaada wowote naomba anisaidie 🥴🙏🏽
qmmke 🤣🤣🤣 pole sana mkuu.pole ndugu yangu mimi nilikosea nkanunua Luku ya 2100000 mwaka jana Mtaa huu nlishafumaniwa ila siwezi kuhama hii nyumba
Masihara bos, kama ni kweli hutakiwi kuungiza hiyo luku unaenda tanesco wanauingiza wenyewe wanaufuta hela inarudishwa, ila siyo zoezi la siku mojapole ndugu yangu mimi nilikosea nkanunua Luku ya 2100000 mwaka jana Mtaa huu nlishafumaniwa ila siwezi kuhama hii nyumba
hujamwelewa mwamba, ishu ya mwaka jana, amesema hawezi hama nyumba japo kashafumaniwa, maana yake kashaingiza kitu inasoma, sasa kama kwa mwez anatumia umeme wa 20k labda, anatakiwa kukaa kwenye hyo nyumba muda gan? na je mwenye nyumba akimpa notisi ya kuondoka je? mtihani huu.Masihara bos, kama ni kweli hutakiwi kuungiza hiyo luku unaenda tanesco wanauingiza wenyewe wanaufuta hela inarudishwa, ila siyo zoezi la siku moja
Si watampunja sana?maana mpaka ije kuisha atakuwa mkononi amepata 80K labda tumuulize kwani mleta mada huo muda wa maongezi ukiangalia unaweza ku-expire?Pole sana mkuu hiyo ni ngumu kumeza. Tafuta mawakala uwauzie
Muda wa maongezi hau-expire. Itabidi afanye hivyo ili arudishe nusu hasaraSi watampunja sana?maana mpaka ije kuisha atakuwa mkononi amepata 80K labda tumuulize kwani mleta mada huo muda wa maongezi ukiangalia unaweza ku-expire?