Msaada: Nimekosea muamala kutuma kutoka Bank, ukaja kwenye simu kama Muda wa maongezi

Msaada: Nimekosea muamala kutuma kutoka Bank, ukaja kwenye simu kama Muda wa maongezi

Ilikuwa ni siku ya jana majira ya Jioni, nikiwa nyumbani niliona bidhaa mtandaoni na nikaipenda nikaamua kuwasiliana na waliokuwa wameitangaza katika mtandao wa Instagram. Nilifanikiwa kuwasiliana nao na nikaomba wanifanyie Delivery hadi nyumbani.

Sasa wakati boda wa Delivery amefika nyumbani, nikawa nataka kufanya malipo yake kwa sababu sikuwa na Cash na nilikuwa na pesa kwenye Bank nikaamua kuhamisha Pesa kutoka Bank kuja kwenye simu ili niweze kulipa kupitia LIPA NAMBA yao na hapo ndipo nilipokuja kukosea badala ya kutuma pesa nikanunua muda wa maongezi wa Tshs 100,000/= 🥴. Pale Pale biashara iliishia pale na nikaanza kutafta namna ya kurudisha pesa imeshindikana hadi sasa

Hivyo naomba msaada kwenu wataalamu nifanye nini? au kama kuna mtu ambaye anahusika nw kutoa huduma za kurusha vifurushi naomba tuwasiliane tufanye biashara nipo tayari ata niingie hasara ya kiasi fulani.
Au mwenye msaada wowote naomba anisaidie 🥴🙏🏽
Haifai kumkatisha mtu tamaa, ila busara sana kumwambia ukweli mtu mapema. Jipange tu namna ya kuishi nazo, hakuna namna zitageuka kurudi tena kuwa hela.

Huo upuuzi niliwahi kuufanya, tena ilikuwa ni hela nyingi zaidi ya hizo na niliishia kutumia na kugawa tu muda wa maongezi hadi ukaisha.

Ova
 
Kenya Safaricom huwa wanabadilisha muda wa Maongezi kuwa pesa. Tanzania kwa sababu ni ncni ya kuchuma tu pesa kwa wawekezaji hilo haliwezekanin na halipo.

Kenya walipiga sana kelele na ndio maana pia bando kwao huwa hai Expire kama huku.
 
Asante kwa kutumia mtandao wa Voda
Salio lako la maongezi ni Shilling 96,000

1720135025596.png
 
Hapa ndiyo wataalamu wa hesabu za mtandao wanafeli. Kimahesabu, issue kama hii ilitakiwa iwe na namna yake ya kurekebisha
 
Masihara bos, kama ni kweli hutakiwi kuungiza hiyo luku unaenda tanesco wanauingiza wenyewe wanaufuta hela inarudishwa, ila siyo zoezi la siku moja
Nilishaingiza na natumikia adhabu m mwaka huu December ndo compensation yangu inatamatika
 
Kwakweli pole tu, mie hadi nilihisi kuumwa🙆🙆
 
Piga deal na muuza vocha wa karibu vocha siku hizi buku na 10 mtu akitaka unamrushia kwa buku muuza vocha unamtoa 5k imeisha iyo
 
Back
Top Bottom