Msaada: Nimekosea muamala kutuma kutoka Bank, ukaja kwenye simu kama Muda wa maongezi

Pole mkuu, hapo ni kuongea na watu wako wa karibu tu unawatumia muda wa hewani kisha wanakulipa maana vibanda vya kupigisha simu siku hizi hakuna na ukikosea kununua muda wa hewani ngoma huwa hairudishwi.

Niliwahi kununua muda wa he wants wa laki 2 mwaka 2012, nilikuwa nawauzia wapigisha simu napo kwa hasara, unamtumia 25,000 anakupa twenty.
 
Uza huo muda wa maongezi hakuna namna ya kupata hela yako zaidi ya kuuza vocha.
 
pole ndugu yangu mimi nilikosea nkanunua Luku ya 2100000 mwaka jana Mtaa huu nlishafumaniwa ila siwezi kuhama hii nyumba
Masihara bos, kama ni kweli hutakiwi kuungiza hiyo luku unaenda tanesco wanauingiza wenyewe wanaufuta hela inarudishwa, ila siyo zoezi la siku moja
 
Masihara bos, kama ni kweli hutakiwi kuungiza hiyo luku unaenda tanesco wanauingiza wenyewe wanaufuta hela inarudishwa, ila siyo zoezi la siku moja
hujamwelewa mwamba, ishu ya mwaka jana, amesema hawezi hama nyumba japo kashafumaniwa, maana yake kashaingiza kitu inasoma, sasa kama kwa mwez anatumia umeme wa 20k labda, anatakiwa kukaa kwenye hyo nyumba muda gan? na je mwenye nyumba akimpa notisi ya kuondoka je? mtihani huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…