Msaada: Nimepata dharura nahitaji Mkopo wa milion mbili, nitarudisha baada ya mwezi mmoja kwa riba ya 20%

Mimi kama mfanyabiasha mstaafu wa kukopesha, wafanyabiashara wengi wajanja viwanja hawachukui, hiyo bodaboda mtu anachukua lakini sio kwa kukupa milioni 2 net, labda iwe mpya kabisaaaa..

Meza mate ya akili, ukikosa kabisa uza pikipiki fanya yako, hela ya kurudisha mkopo ununue tena pikipiki yako. (wazo la nyongeza)
 
Mkopo ni 30% interest kwa siku 30.
 
Wakopeshaji nao WENGI walisikia dhamana Fulani Nia Yao SIO msaada...Bali watanufaikaje na hiyo dhamana , inakuwa Kama unawauzia tu...kuna MTU alichukuliwa gari Kwa 1.5m ilihali thamani yake si chini ya 5ml...LAKINI alifurukuta Sana kurejesha wapi..na Bora wangekuwa WANASEMA ukishindwa tunauza ..Kila mtu achukue chake...anyway tunajifunza pia kuhakikisha tunajiunga ktk mifumo ya pesa za kukopa kirahisi kama vikoba nk.
 

Mungu akujalie ufanikiwe. Mikopo mingi ya namna hii kwanza anaekupa anakesha kuomba na kusali ushindwe ili aweze kutaifisha mali zako [emoji17][emoji17]. Utafanikiwa inshaallah.
 
Iyo bodaboda unamaanisha nitakuwa nikiiyangalia tu au unaniruhusu niitembelee au nakaa na kadi?

Pia nataka kufahamu kama ukishindwa kurudisha je tunataifisha hizo dhamana?!!!
Kama uko tayari nashida na mkopo wa 700,000 dhamana ni kadi ya gari nitarudisha 1,000,000 kwa miezi 5
 
Ungekuwa unauza hicho kiwanja angalau ila kukopeshana hapana
Ila ukitatua changamoto zako nitafute uingie sehemu ambayo ikiwa na dharura unapata ela
Ukiitaji mtaji unapata ela
Sehemu hiyo ni ipi na ina vigezo gani kuingia...am interested
 
Wenye hela hawana huruma na wenye huruma hawana hela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…