Msaada- Nimetapeliwa Kariakoo- Vitasa 100 feki za milango sawa na TSH 2.3million

Entim

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
4,025
Reaction score
2,261
Salaam wana Jamvi,
Katika hali ya kushangaza, picha hapo chini ni kitasa chamlango wangu nilionunua wiki 2 zilizopita. Kariakoo, risiti ninazo (TZS 100@230,000=2.3million). Cha kushangaza ni kwambazinasambaratikavyenyewe(bila kugongwa). Cha kushangaza niliporudikwa muuzaji badala ya kunionea huruma, ananiambia risiti imeandikwa maliikishauzwa hairudishwi, ilibidi niwe mpole kama mama lishe!!
Msaada: Naombeni msaada sehemu muafaka/dukana aina ya kitasa imara nay a kudumu kabisa, hata kama ni expensive siyoissue(quality speaks better than quantity).
 

Attachments

  • Kitasa.jpg
    7.2 KB · Views: 1,049
Hivi inakuwaje mkishapigwa na mnakuja kuweka post?ilikuwa na kizuizi gani kabla ya kununua ungeweka post kuwa unatafuta vitasa?kuna wana jamvi humu wana maduka na wangekushauri aina bora ya vitasa na sio "bora vitasa" Pole lkn kwa ushauri nenda polisi kuna sharia inayoruhusu kurudisha mali dukani baada ya kununua hizo risiti zao na longo longo wala lisikutishe
 
duuuuu ndio maaana mimi kabla ya kununua nmeamua kupata maujuzi kwanza pole mkuuu
 
Viunganishe na supagulu.
kuna wakati tunatakiwa kujitambua. jf ina majukwaa mengi na naamini yanakidhi mahitaji ya wengi. Kuna jukwaa la jokes etc nadhani ndo lingefaa kwa post yako iyo. Big uo s.crony pia na mimi nimeelimika kwa post yako... Pole sana mtoa mada kwa yaliyokusimbu, fuata ushauri wa mdau hapo juu
 


Mkuu Nchi hii ni yetu sote! Uozo kama huu lazima tufike mahali kuuondoa kama si kuumaliza lakini hata kuupunguza.
TSh 2 .3ml ni pesa nyingi kupotea hivi hivi kwenye bidhaa feki.Tafadhali peleka Bidhaa hiyo feki TBS na Chama cha walaji ilikuepusha kuumizwa kwa mtu mwingine huu mtandao wa bidhaa feki wananeemeka na kupata utajiri wa haraka.



NB. Mkuu Invisible kwa hisani yako naomba kuwasilisha ombi usaidie MODS kufikisha Maombi ili kama inawezekana hawa jamaa wa TBS wakawepo humu JF ili mambo kama haya tupate mahali pakusemea pengine itasaidia Jamii.




 
Last edited by a moderator:
Hata kama mali ikishauzwa hairudushwi ndio aniuzie feki? naanza naye peleka tbs naye wamfilisi kisha mfungulie kesi ya mafai.
 
Viunganishe na supagulu.


Acha mawazo ya Kibange bange! Siku yakikupata ndiyo utajua wafanya biashara ni watu wa aina gani!.
Ndiyo maana jamii imeoza kweli kweli mawazo kama hayo imagine unarithisha mwanao huyo mtoto yeye itakuwaje?
 
Acha mawazo ya Kibange bange! Siku yakikupata ndiyo utajua wafanya biashara ni watu wa aina gani!.
Ndiyo maana jamii imeoza kweli kweli mawazo kama hayo imagine unarithisha mwanao huyo mtoto yeye itakuwaje?

Achana nao watoto hao, kura kurara bure!
 
Pole asee siku ingine uliza kwanza Dar wamejaa wahuni wengi na matapeli.
 
Hili suala halikubaliki jaribu kulifuatilia kwa hawa watu wa TBS, hiyo hela sio haba, nachukia sana kununua vitu standard pale kariakoo.
 
Kama mdau alivyotaja hapo juu kuhusu kwenda TBS, usifanye mzaha, hawa watu wataendelea kucheza na uvivu wetu wa kufatilia haki zetu kama tutaendelea kutojitambua.

Nenda TBS, wakishindwa fungua kesi ya utapeli/madai. Nina uhakika atashikishwa adabu. La sivyo aanze kuripotiwa kwenye mitandao ya kijamii ili watu kupeana tahadhari, muhimu ni kwamba uwe umesha tolea taarifa kwenye vyombo husika.
 
mkuu pole sana nakushauri usikubali iishie hivi ivi,na ikiwezekana tuwekee wazi hilo duka tulifahamu.
 
Viunganishe na supagulu.

Riuzaji bidhaa feki hiri hapa! TBS waje waanze naro humu humu JF! Mtu gani hujui wapi pa kuwa serious na wapi pa kuropoka! Action equals to reaction, ngoja ikukute na wewe!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Kuna sheria zinazokulinda na hali kama hiyo Tanzania, kuna mwanasheria alianzisha "Tanzania Consumer Advocacy Society", fata hii blog na jaribu kuwasiliana nae utapata ufumbuzi, huyo mwenye duka atakulipa gharama zako zote, za usafiri, uchukuzi, ununuzi, ufundi, muda na hasara zilizokupata kwa kukuuzia vitu vibovu, na si za ununuzi tu:

TANZANIA CONSUMER ADVOCACY SOCIETY

Nchi za nje mawakili huwa wanazinunua kesi namna hii huku wanashangilia, nashangaa hapa Tanzania mawakili wetu hamchangamkii ulaji wa uhakika huu.

Naona kama hesabu yako umekosea hapo, hebu rekebisha.
 
Vitasa 100@230,000/= ndo jumla ukawa umetapeliwa million 2.3?
Kumbe ndio maana huyo jamaa akakuibia
 
Sheria ya mkataba inakulinda kwa nguvu nyingi sana. kwa maana ili mkataba ukamalike kuwe na free consent(uhiari),lawful object or lawful consideration,intetion to create legal relation.katika hiyo issue yako kimepungua lawful object na free consent hivyo kuna zaliwa kesi ya madai au kesi ya jinai. fuata sheria ushinde.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…