Msaada- Nimetapeliwa Kariakoo- Vitasa 100 feki za milango sawa na TSH 2.3million

Nenda ubungo plazza kaulize FCC,fair competition commission,ina fanya kazi na ku mtetea mraji,mi niliuziwa flash feki mwaka 2012,nilienda tbs,tbs wakaniambia niende hapo,nilipoenda wakanipa barua niwapeleke walioniuzia flash fake ikisema wanipe hela au wanibadilishie,wakanikatalia kurudisha hela hata kubadilisha,nikaenda kutoa taarifa tena,ndipo nikaondoka nao kutumia gali lao hadi kariaokoo,kufika pale wakaawaambia either wanipe hela yangu au watoe faini milioni mbili,wale jamaa wakaamua kunirudishia hela yangu yote.
kama upo serious fanya hivyo,wewe nenda pale ubungo plaza kaulizie ofisi za fair competiton,watakusaidia,walikuwa hawanijui,wala siwajui,ila walinisaidia kupata haki yangu.
 

Mkuu umeandika kama unakimbizwa? M nmeelewa vitasa umetapeliwa, sasa unata urudishiwe fedha japo rist imeandikwa hairudishwi mali aliyo nunua au mahali pa kupata vitasa?

Nextime, usiende mwenyewe kununua mpe fundi anaekujengea utapata vitasa vyema.. Au nenda mliman city hapo utapta mpaka warrant,

Pole kwa kupigwa hyo ndo bongo, ww umelia wenzio wamecheka, haya maisha bwana yaache tuuuu..
 

Uelewa wa consumer protection hapa kwetu upo chini sana sana. Wanasheria nao sio wabunifu kupanua wigo wa aina za mashauri wanayochukua, hawatoi ushaurikwa wananchi kuwa wana haki kama hawapati huduma muafaka kwa hela wanayolipa. Mifano michache ni kama insurance claims ukiangalia kwa kina utakuta wanaolipwa ni wachache na hao wanaolipwa kiasi ni kidogo sana kulingana na maumivu wanayoyapata.

Kila siku tunanuna airtime ni wachache sana mingoni mwetu twaweza kuthibitisha kuwa kiasi walichotumia ndicho walicholipia. We dont question and kife goes on and the kampuni za simu get richer and richer.

Tunanunua umeme in advance halafu provider anakupa umeme anavyotaka yeye, kwa nini iwe hivyo akichukua hela yake ni LAZIMA AKUPE UMEME asiseme kuna mgao.

Unanunua bia baa kwa bei ya 500 ml unaambiwa hawana na badala yake wanakupa ya 300 ml ukinywa bia tano za 300 ml na ukiwa unapigwa kihivyo utakuwa umepunjwa bia 2 za 500mls and we dont complain.

Mifano ni mingi sana haina mwisho. Something has to be done.
 
Last edited by a moderator:
Nenda pale mwenge itv, asa abloy, wanauza vitasa vya union, hao ndo wakala wa union
 

Ushauri wa kwenda Polisi ni mzuri kabisa. Lakini ushauri wa kuuliza kwanza jamvini ni mgumu. Tutauliza vingapi na mara ngapi? Kuna uhakika gani utapata ushauri mzuri?
 

Faiza hii society kama ipo basi vision yao ni ya kizamani sana hawajitangazi yaelekea ni watu wa ofisini na mitandao hawaendi field ambako ndipo uonevu ulipo.

Hata hivyonimwanzo mzuri.
 

Dah, pole mkuu. Mara zote unaponunua ulizia guarantee, manufacturer wengi ambao ni legit wanasimamia bidhaa yao hata 2yrs, na hiyo guarantee iwe imeandikwa na terms zake ziwe wazi. Ukiangalia brands peke yake bado utalia kwa sababu hawa matapeli wanaojiita wafanyabiashara wanakwenda china na kuclone brands maarufu. Na huyo usimwache, nenda TBS karipoti na ufuatilie, nadhani kuna mamlaka nyingine inayotetea walaji lakini sikumbuki ni mamlaka gani, hakikisha unafuatilia suala hilo, not only for the 2M, lakini kwa ajili ya kupata haki kwa mujibu wa sheria.
 
Cheap has always been expensive!!!!!

You must be joking 230,000tsh per pc = 143Us Dollar (Rate of 1600tsh) and you still call Cheap ! Anway human being have different income levels but aleast for average Tanzanian for this price you expect better quality.
 
Hapa ndipo ninaposhauri watu wajifunze kutumia vitu vyenye nja kali...Mrudishie mali kabla hujamwambia chochote chomoa hii kitu..
 
kaka wasikukutishe tamaa baadhi ya watu humu. Amka nenda TBS watakusaidia ukiona wanalongolongo nyingi ujue wana issue nayo hilo duka. usichoke nenda karipoti police ili hatua za kisheria zianze za kulinda usalama wako kwanza then nenda ukafungue kesi ya madai mahakamani utalipwa pesa yako na fidia juu. Chonde chonde kaka usikae kimya wasaidie wengine wapo wengi sana wanaoliwa lakini hawasemi pia ebu saidia jamii kuonesha tumechoshwa na bidhaa feki.
 
You must be joking 230,000tsh per pcs = 143Us Dollar (Rate of 1600tsh) and you still call Cheap ! Anway human being have different income levels but aleast for average Tanzanian for this price you expect better quality.

"Cheap" in this aspect doest not necessarily mean "Many digits" rather it implies "easily available"


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Faiza hii society kama ipo basi vision yao ni ya kizamani sana hawajitangazi yaelekea ni watu wa ofisini na mitandao hawaendi field ambako ndipo uonevu ulipo.

Hata hivyonimwanzo mzuri.

Wangekuwa hawajitangazi mimi ningewajuwa?

Hao ni watu binafsi waliojitolea, kawasome, nimeweka link ya blog yao, na ukiweza na wewe unaweza kuwatangaza kwa faida yako na wengine kama nilivyofanya mimi.

Msingoje kila kitu kufanyiwa.
 
Inabidi uwe na fundi wakati unapotafuta vifaa kama hivi, la sivyo utakuwa mnunuzi kila siku.
 
Wangekuwa hawajitangazi mimi ningewajuwa?

Hao ni watu binafsi waliojitolea, kawasome, nimeweka link ya blog yao, na ukiweza na wewe unaweza kuwatangaza kwa faida yako na wengine kama nilivyofanya mimi.

Msingoje kila kitu kufanyiwa.

Wewe ni kati ya wachache unaowafahamu, wengi waliobaki hawawafahamu na kufanya iwe ngumu kupeleka malalamiko yao.

Ofisi zao ziko wapi ili tusaidie kuwatangaza, maana kwenye blog yao hawaoneshi wanapatikanaje.
 
Wewe ni kati ya wachache unaowafahamu, wengi waliobaki hawawafahamu na kufanya iwe ngumu kupeleka malalamiko yao.

Ofisi zao ziko wapi ili tusaidie kuwatangaza, maana kwenye blog yao hawaoneshi wanapatikanaje.

Fata blog na waandikie, au unaweza pia kutumia google kuwatafuta au unaweza kwenda BRELA ukapata habari zao zote kwani wamejiandikisha rasmi kama wanavyoeleza kwenye blog yao, kwani kwa sasa na wewe umeshawajuwa kuwa wapo.

Usingojee kila kitu kufanyiwa.
 

mkuu kwa hesabu hizo utakua hujatepeliwa.au labda iwe ni makosa tu yakimahesabu.
 

Mkuu vilikuwa 10 au 100? Maana hesabu yangu imegoma kabisa! Labda kama vilikuwa vinauzwa 23,000/= Turekebishie kwanza hapo mkuu ndo tuendelee!!
 

Mkuu,umenistua kweli,hiv tunaongozwa kwa SHARIA au sheria au ulimi umeteleza mkuu,
 
Watz. hupoteza hela nyingi kwa kutapeliwa bila kujua lakufanya. Wakati mwingine ni kudharau mambo madogo madogo. Utakuta mahali pamendikwa usikojoe hapa, halafu unaona mtu anafanya kinyume chake.

Nilikuwa kwenye mkutano wa shule ya mtoto wangu. Tukaambiwa kuna wazazi wengi tu wametoa hela cash kwa mhasibu, na sasa kakimbia. Instruction ni kwamba shule haipokei cash. Sasa wanaambiwa hawajalipa ada wanashangaa . Hata risiti ikiandikwa vile ,haina maana uuziwe boya. Una haki ya kurudishiwa hela yako. Risiti ya TRA haiandikwi upuuzi kama huo. Nenda akupe risiti ya TRA.
 
Assa Abloy wako hapo mwenge kanunue kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…