Msaada: Nimetengeneza gari lakini ukiendesha inasikika harufu ya mafuta

Dormant Account

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2022
Posts
11,308
Reaction score
32,757
Nina Gari nimetoka kuitengeneza ilikuwa inaonyesha check engine wakanambia mikolokolo kibao wakatengeneza Ile check engine ikatoka kwenye dashboard sasa nimeendesha kama siku 4 hivi ukiwa ndani ya Gari unasikia harufu ya mafuta kabisa.

Jana nawasha nikadhan mafuta nikasema ngoja niweke nikaweka ya 50000 nawasha yani mpka ukanyage mafuta kwa nguvu ndyo inawaka nikatembea ikafika sehem ikazima kuwasha mpka ukanyage mafuta kwa nguvu.

Tatizo itakua nini?
 
Gari gani? Nahisi pump ina shida hapo. Ebu peleka kwa mafundi wanaojielewa.
 
Cheki ignition coils na spark plugs..!
 
Plug feki
Angalia coil au pump pia huenda fuel system ina leakage mahali cheki uvujaji
 

Mafuta hayaungui hayo mkuu.

Check engine imepotea au wamenjunga?
 
Mafuta kuungua ndyo inakuaje maana mm siyo mzoefu wa magari
Mafuta yanaungua ndani ya engine ndio maana unaona magari yanatembea barabarani.

Sasa yakiwa hayaungui vizuri ndio inaweza kupelekea wewe kusikia hiyo harufu.

Zipo sababu nyingi zinazoweza kupelekea hiyo shida. Hiyo check engine huenda wamezima tu taa na siyo kurekebisha tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…