Msaada: Nimuoe huyu binti au nisikilize ushauri wa Wazazi wangu?

Kwenye kuoa mwenye maamuzi ni wewe bhana
 
Haya ndio matunda ya uasherati. Nyakati kama hizi huja. Kama ulijua ana mtoto na wanalea mtoto wao, na wewe ukaona sio tabu ukaweka mbegu, leo unasema kulea mtoto wa mwenzio ni ngumu?
Oa huyo mwanamke maana hujajua tu ni uchungu kiasi gani utamsababishia kuachwa tena.

Hakikisha mambo yaliyosababisha wao kuachana unayafanyia kazi ili isitokee kwako. Wazazi tunawapenda ila wakati hufika maamuzi yao huwekwa kando. Ukichunguza pia familia nyingi ambazo walianza fresh, ndani yake kuna usaliti, na watoto wasio wa ndoa husika pia. Kama hakuna ya ziada uliyoficha, mchukue huyo mwanamke
 
Mkuu, neno sahihi ni mama
Unakipotosha Kiswahili kwanini amuite mama wakati ni binti mwenye ujauzito wake? Ni afadhali amuite binti tu. Kumuita mama/dada sio sawa wakati anapiga!
 
Nisikilize mimi kama umeamua kutosikiliza wazazi,
KAA MBALI NA WANAWAKE WENYE WATOTO,
NARUDIA KAA MBALI
hakuna kitu utafanya kwa mwanae aone ni sahihi na changamoto kubwa ni ambavyo hiwez lea mtoto asie wako.
Bro kaa mbali i mean it
 
Achana naye haraka sana.Huyo siyo wa kuoa ni chapa ilal tu
 
Huu ushauri wako leo ingekua ni 80's ama early 90's ungefanya kazi ila kwa kizazi hiki bora achukue mwanae alee kuliko kuoa mwanamke mwenye mtoto,
Najua changamoto zake ndo mana simshauri hata kidogo,
 
Itafute Sana Aman uifuate
 
usikilize moyo wako ndipo uamue,ama kuhusu mtoto,mruhusu aende kwa baba yake mzazi,hizo alinacha zingine achana nazo
 
Wanaume tunazidi kujushisha thamani sana miaka hii. Inasikitisha sana

Hivi unaanzaje kuzaa au kutaka kumuoa single maza, baby mama wa mwanamume mwingine?

Haijalishi umezaa naye au haujazaa naye single maza sio wa kuoa na kufanya naye maisha. Acha huo ujinga USITHUBUTU

A man should start his own family, not join another man's family
 
Ndugu yangu kwenye hilo suala sikiliza wazazi wako,narudia tena sikiliza wazazi wako aisee yasije yakakukuta mazito huko mbele ya safari
 
Lakini Mimi suala la kulea mtoto WA mwanaume mwenzangu naona itakuwa fedhea sana kwangu.
Umeshayatimba. Huwezi kutofautisha matunzo ya mama na mtoto wake. Baba wa mtoto mwingine akishindwa wewe utawajibika kwa kujua ama kutokujua
 

Muoeni wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…