Msaada: Nimuoe huyu binti au nisikilize ushauri wa Wazazi wangu?

Sasa muda wote unaruka nae dhamira yako ilikuwa ni ipi kwake?

Ulikuwa unalala nae kupunguza upwiru?

Ulikuwa unalala nae sababu umelogwa na haujui mwanamke wa kuanza nae maisha utampata wapi?

Ulikuwa unalala nae ili kutest utamu?

Shida huwa ni nini?

Kwann unaanza mahusiano na mtu ambaye ukiambiwa kesho mfunge ndoa awe mkeo wa maisha roho na akili vinakugomea.

Me nadhani ifike wakati sasa ukikuta mwanamke haeleweki na unaona kabisa hana sifa za kuwa mke then umkalie mbali. Kama unataka kupunguza hamu tafuta hawa wakujiuza ili kupunguza hii kasumba ya kuzalisha wanawake ambao hautaweza kuishi nae.

Mnatutesea hawa Malaika mnaowaleta kwa maamuzi ya kibinafsi sana halafu wanakuja kukuta baba na mama hawana akili ya maisha ya pamoja wapo wapo tu wanaanza teseka na kukosa upendo na attention ya baba na mama.

Mimi nawaonea huruma sana na kujiskia vibaya sana watoto hawa wasio na hatia mnawafanyia huu ukatili. Ipo siku mtalipia haya mateso mnayowapa hawa watoto.
 
Mleta mada ishi humu, achana na mawazo ya wazazi ila kaa hapa.
 
Ninadhani wazazi wako ni members wa JF pia. Jitahidi kusoma comments zote labda unaweza kugundua ID ya mzazi wako. Msimamo wa wanaJF ni kama wa wazazi wako.
 
Huu ushauri wako leo ingekua ni 80's ama early 90's ungefanya kazi ila kwa kizazi hiki bora achukue mwanae alee kuliko kuoa mwanamke mwenye mtoto,
Najua changamoto zake ndo mana simshauri hata kidogo,
Umewahi kupitia changamoto zipi watu wajifunze?

Ningependa tufahamu walau kupata abc
 
Mechi imeanza 1-0 sema si umesema ana kiumbe chako kakibeba basi akijifungua 1-1. Hapo pambana utafute goli la ushindi.
 
Sasa ndugu kama umeona wazazi wanaongea pumba kwasababu ya genye zako,utaweza kuwasikiliza wana jf usiowajua kweli....!!! Baba na mama yako ndio nguzo yako
 
Nimekuelewa Kwa herufi kubwa Mkuu.
 
Halafu mbona kuna wanawake wengi tu ambao hawajazaa?

Unakwama wapi Mkuu?
Ishu sio kuzaa au kutokuzaa Mkuu, unaweza ukaja ambaye ni fresh hajazaa ila akawa anapasha kipori na ex wake. Nafikiri point ya msingi ni namna ya kudhibiti mawasiliano kati yake na na baba mtoto wake
 
Kwenye kuoa mwenye maamuzi ni wewe bhana
Ni kweli mm NDIYE mwenye maamuzi lakini BILA baraka za wazazi pia, haitakuwa ndoa yenye afya. Hata Kwa Sheria za ndoa Ili ndoa iwe halali lazima wazazi waridhie.
 
Ishu sio kuzaa au kutokuzaa Mkuu, unaweza ukaja ambaye ni fresh hajazaa ila akawa anapasha kipori na ex wake. Nafikiri point ya msingi ni namna ya kudhibiti mawasiliano kati yake na na baba mtoto wake
Ex wanaweza kuachana na wasitafutane tena. Huo uwezekano upo

Ila Wazazi hawaachani Abadan.
 
Nimeishia hapo ana mtoto mmoja, ila anya way nakushauri sikiliza wazazi
 
Kweli mkuj Single mother siyo wanawake wakufanya nao maisha, huyu ili alijue ilo anatakiwa atafute binti ambaye hana mtoto ili aone tofauti ya kimawazo na Marengo. Mwanamke mwenye mtoto akili yake ni kujenga uchumi wake na wa mtoto wake, Binti akili yake ni kujenga uchumi wa wote kwa faida ya uzao wenu.
 
Umesema vyema
 
Yaani una mashaka na ushauri wa Malegend...

Mtoto akililia wembe, mpe....
 
Ukiwapenda dagaa huwezi kukwepa kutafuna mchanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…