Msaada: Nina appetite iliyopitiliza

Msaada: Nina appetite iliyopitiliza

MBITIYAZA

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2017
Posts
14,947
Reaction score
26,074
Jaman nadhani kuna watu wa design kama yangu mie mbinti !Jamani mie nimekuwa napenda kula kula vitu viduchu duchu mnoo !yaani nahisi kuna kitu si bure ! imefikia hatua sikosi kitu cha kula kula, vitu navyopenda sana ni vya sukari sukari ubuyu, bites, popcorn za flavor nzuri na sukari !yaani niliamua kujitune nile matunda nikawa najihisi njaa tu, nikahamia kwenye maji nikaona uzushi yananifanya nile zaidi yaani nikikaa bila kula kula najihisi sipo okey kbs! sina mwili mkubwa sana but nanenepa kiwango cha lami

Nikiwa home weekend ndo kabisaaa !naingia kbs jikoni kupika pika napendelea zaidi kubake ,kufry na kutengeneza smoothies basi ikinijia picha ya samak/au nione nyama nzuri sehemu lazimaaa aisee nitajitahd nipate samaki, nyama nikaange nile, hapo saa 10 utanikuta jikoni natengeneza samosa za pilipili nile au nitatengeneza kitu chochote tu mradi niwe na vifaa !uwiii jamani mbona nahisi kuchoka na siipendi hii tabia?? na mume nimemuambukiza basi uwii nakesha jipikilisha tu !

Madaktari msaada wenu nawezaje acha hii tabia yaani nataka niwe nakula atleast mara 4 tu kwa siku !!!!!!!!!! nikate kabisa ice creams na mazaga zaga yake !nataman kuhamia kijijini ambapo hata unga wa ngano ni adimu au matunda yasiwepo !

cc Miss Natafuta aka miss papa!mpenda kula kama mie
 
yaani huwezi amini nilitaka kuleta uzi kama huu.mimi simalizi masaa mawili bila kutafuna kitu.yaani nakula mdogomdogo kama mchwa.siwezi kula lisahani hilo.ila yaani nakula kula sana
 
hiyo ni dalili ya unene kukujia, mtu ambae kilo huanza huongezeka, dalili ya awali kabisa ni kupenda kula kula na kupatwa na njaa mara kwa mara
 
yaani huwezi amini nilitaka kuleta uzi kama huu.mimi simalizi masaa mawili bila kutafuna kitu.yaani nakula mdogomdogo kama mchwa.siwezi kula lisahani hilo.ila yaani nakula kula sana

Haaaaaaaaah hv hapa nina popcorn jaman nazifata mbali nyie, kuna kaka anazitengeneza nzuriii za tangawiz bas mie kila siku nikifika pale namwangaliaga tu ananifungia najisepesha !leo sijenda kazini huwz amini nimezifata mjini !uwiii !hapana sio kawaid jaman na wala sio minyoo !

kuna dada mmoja job yy halag kitu jaman zaid ya lunch !ananiambia nina PEPO niende naye kanisani hahahahahha !
 
yani unajikuta unapenda kula kidogo kidogo ila mara nyingi nyingi kwa siku
 
Nimekuja kasi sana kwenye huu uzi nikajua ni appetite ya ngono, basi sawa, usile sana, too much is harmful.

hahahhahah aisee nimecheka !sure mkuu ila sasa jinsi ya kuacha ndo nashidnwa
 
unaona eeh! mimi mwenyewe hali hiyo ilinikuta, nikaambiwa ni dalili ya uzito kuongezeka, nikaanza kuacha taratibu hadi sasa kilo zangu nime maintain

ukipata na njaa ulikua unakula nn sasa !mie siwez kbs kushinda na njaa hata kuongea huwa kunakata
 
hahahhahah aisee nimecheka !sure mkuu ila sasa jinsi ya kuacha ndo nashidnwa
Yeah, if its habit now, its hard to get out of it, but kaa mbali na chakula, kuna msemo i picked it somewhere " unapaswa kula chakula kama dawa sasa, ili usije kula dawa kama chakula baadae"
 
ukipata na njaa ulikua unakula nn sasa !mie siwez kbs kushinda na njaa hata kuongea huwa kunakata
nilitajiwa vyakula vyenye calories chache mfano matunda , niliambiwa nikila hayo hata idadi ikiwa kubwa siwezi ongezeka kg
 
Haaaaaaaaah hv hapa nina popcorn jaman nazifata mbali nyie, kuna kaka anazitengeneza nzuriii za tangawiz bas mie kila siku nikifika pale namwangaliaga tu ananifungia najisepesha !leo sijenda kazini huwz amini nimezifata mjini !uwiii !hapana sio kawaid jaman na wala sio minyoo !

kuna dada mmoja job yy halag kitu jaman zaid ya lunch !ananiambia nina PEPO niende naye kanisani hahahahahha !
asubuhi nimekunywa kikombe cha uji wa lishe
saa nne nikala mkate slace moja na bakuli la tikitimaji
saa saba nikala wali nyama robo sahani
saa nane nikala samaki mdogo mmoja wa kukaanga
hapa nakula tende na maji
 
Back
Top Bottom