1. Mwendokasi utasaidia wewe kusave sana hela. HOW?
Kwanza fuata vibao vya barabarani. Kwenye 50KPH tembea speed hiyo hiyo ili usigombane na matrafick Wakachukua 30,000TSH zao. Na unaporuhusiwa above 50KPH tembea kati ya 80KPH to 120KPH. Usitoke kwenye hii range. Hapo ulaji wa mafuta utakua ni minimum. Vioo ukiwa umefunga. Vilevile angalia braking na acceleration zako. Usikanyage sana wese ili ukoleze gari mapema. Wese linaenda sana pale. Na epuka braking za ghafla. Unachakaza gari na hatari.
Kwahiyo speed ni muhimu kwa afya ya chombo, gharama na usalama wa wasafiri.
2. Mafuta lita 50 more than enough. Tukiassume una 2.0L car kwa hizo kilometer 350 za Dar to Tanga kwa hiyo gari ikiwa na consumption ya 10KM/L utatumia lita 35 tu. So utabakiwa na lita kibao tu za Misele. But kumbuka service ya gari, uendeshaji wa dereva (especially hapo kwenye acceleration ) kutachangia sana ulaji wa wese.
3. Huo umbali mfupi sana. Kanyaga moja kwa moja. Stop and go zinaongeza ulaji wa mafuta sana. Kwahiyo piga moja kwa moja.
Additional:
4. Ondoka mapema sana kama saa 10 asubuhi. Ukiondoka saa 12 utakua unafanya racing na mabasi ya mkoa. Sio viunbe wazuri wale.
5. Pitia njia ya Bagamoyo. Ni fupi zaidi. Kama huijui vizuri, tumia Google Map. BTW huwezi kupotea.
6. Kama mtakua wawili itakua poa zaidi. Njiani mambo mengi.
7. Usipige vichwa. Ile kuokota abiria wa njiani. Ondoka na mtu unaemjua kutokea DSM.
8. Usalama kwanza. Seat Belt, Usitumie simu huku unaendesha.
All the Best Bro.