Msaada: Nina safari ya Dar-Tanga, nataka kutumia RAV4 old Model

Tungekuwa na asilimia 50% au zaidi ya members Wa jf wenye michango ya namna hii watanzania tungekuwa tumefika mbali sana kisaikolojia na kimaendeleo... Big up!!
 
Mkuu kwa kawaida GX100 yenye engine G kavu inatakiwa kutumia litre moja kwa KM ngapi? Je, plug (let's say Denso) za meno matatu ni bora zaidi kuliko za meno mawili au moja? Tofauti ya hayo meno ni nini?
 
Kupumzika sio mbaya. Unaweza ukatoka Dar mpaka Chalinze. Ukifika pale vuta pumzi dk kumi na tano, tafuta kinywaji chako cha Azam Energy au Mo energy baridi piga kuondoa uchovu. Then nyosha goti mpaka Segera. Ukifika pale tena vuta pumzi dk kumi, nunua nunua matunda pale huku ukivuta pumzi. Then baada ya hapo tena nyoosha goti mpaka Tanga.
 
Mbona tanga karibu sana mzee? Kua makini na alama za barabarani... Speed nzuri ni 100-120 km/hr
 
1.Andaa hela ya trafiki tu kama elfu 60 uwashikishe elfu5 kila wakikudaka just incase maana inaonekana hata Tanga hupajui.

2.Gari iwe full tank kukwepa usumbufu wa sheli na ufunge mkanda kabla hujaingia highway.

3.Usisahau kubeba spare tyre, jeki yako na maji na usali kabla ya safari.

4.Kupumzika sio lazima maana gari ya Rav 4 ina radiator cooling technology. Labda kama utajiskia uchovu sana ila roughly ni safari ya masaa 5 toka dar.

5.Usile chakula kizito (wali,ugali) kabla ya kuanza safari, digestion in tabia ya kuleta usingizi hasa majira ya mchana.
 
nilishaondoka na gari kama hiyo hadi kahama, non stop, wewe unaongelea Tanga?
Si ndo maana ameomba msaada. Wewe mzoefu na magari au safari ni kiasi cha kumpa maelekezo tu afanyeje..!
 

Sante Kwa ushauri bro
 

[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Sharo milionea aliponunua gari aliuliza hivihivi ingawa Safar yake iliishia korogwe
 
Zingatia sana vibao vya speed 50.

Hakikisha una hela za chenji ndogondogo incase kama trafik akikushika speed.


Mm last week nlienda arusha nikatoa buku 8 tu njiani kuna sehem nlijisahau speed wakanipiga toch mara 2.
Mmoja akala buku 5 na mwingine akala buku 3
 
Sharo milionea aliponunua gari aliuliza hivihivi ingawa Safar yake iliishia korogwe
Korogwe tena!!!

Alipata ajali maeneo ya Muheza kama kumbukumbu zangu zipo sahihi...
 
A) Mwendokasi 100-120km/hr
B) 55ltrs yaani full tank utafika yakiwa yamebakia robo tank
C) Ukipenda japo siyo lazima unaweza nyoosha moja kwa moja

NB. Tochi, kwny 50 tembea 50
Asisahau kusimama kwenye michoro ya pundamilia
 
Gari kama MarkII Grande yenye cc2500 inaenda Dar na kurudi TA ikiwa full tank, so am assuming RAV 4 yenye ~2000cc ikiwa full tank itafanya the same...

yah ninatumia 2.4L engine natoka Moshi hadi Tanga na kurudi lita 70
 
Safi sana mkuu, umefafanua vzr sana,
Pia check tyre pressure, Mimi natumia gari kama hiyo, mbele naweka upepo 35 nyuma 40 nakuwa very comfortable.

Usisahau kuwa na spare tyre
Triangles
Jack
Fire extinguisher
Wheel spanner
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…