Msaada: Nina tatizo la kumchukia mtu wa jinsia yoyote anayefanana na adui yangu kwa sura

Msaada: Nina tatizo la kumchukia mtu wa jinsia yoyote anayefanana na adui yangu kwa sura

iamriq_arthur

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2021
Posts
440
Reaction score
1,086
Natumai mu buheri wa afya tele,

Bila kupoteza wakati, naombeni tiba ya kutatua tatizo hili.

Nina tatzo la kumchukia mtu yeyote nnayekutana nae barabarani anaefanana na adui yangu ama mtu nisiyempenda naye ntaanza kumchukia hapo hapo.

Yaani haijalishi kama hajawahi nikwaza ntamchukia hivyo hivyo kwasababu amefanana na adui yangu ambae tulishakwazana kitambo.
 
Kwa vile ni chuki tu na huwadhuru basi endelea.
Usijikoroge ukamvaa mtu kisa kafanana na unaemchukia, utaishia kula makonzi ya ugoko.

Halafu ikiwa hujawahi umba hata kipepeo, unapata wapi ujasiri wa kuchukua binadamu mwenzio?
Unajua kuwa chuki ni matumizi mabaya ya hisia?

Kuchukia mtu haijalishi kakufanyaje, kunamithilishwa na kunywa sumu huku ukitarajia unaemchukia ndio adhurike.
 
Me pia natamani niwe normal hii hari initoke ndio maana nmekuja hapa jukwaani kuomba msaada wa ushauri jinsi ya kuachana na hari kama hii
 
Natumai mu buheri wa afya tele,
Bira kupoteza wakati, naombeni tiba ya kutatua tatizo hili, nina tatzo la kumchukia mtu yeyote nnaekutana nae balabalani anaefanana na adui yangu ama mtu nisiyempenda naye ntaanza kumchukia hapo hapo wala haijalishi kama hajawahi nikwaza ntamchukia hivo hivo kwasababu amefanana na adui yangu ambae tulishakwazana kitambo.
Kwa nini uwe na adui
 
Next time tembea barabarani usipite huko balabalani.
 
Ni umaskini tu wakati mwengine unaotusumbua sisi maskini mpaka tunadhani tuna hasira kumbe hakuna kitu kama hicho.

Mtu hunijui sikujui wala sijakusemesha kukuomba kitu natembea kwenye barabara ya umma wewe from nowhere unichukie kama siyo njaa na hela huna ni nini?
 
Chuki ni kinyume Cha upendo ..mi nadhani . ukiwa tayari kuachilia vitu moyoni na kumsamehe utakuwa sawa.
 
Back
Top Bottom